Kalenda
ya Ufugaji Nyuki ni mwongozo kwa Mfugaji Nyuki kujua majira katika eneo
analofugia ili kuweza kupanga ratiba ya kazi za kusimamia makundi ya
Nyuki.Katika nchi za kitropiki kuna
vipindi vya kiangazi na vipindi vya mvua sio kama nchi za baridi ambapo kuna majira ya vipindi vinne kwa mwaka.Kalenda ya
Ufugaji Nyuki Tanzania imegawanyika katika misimu minne kulingana na majira kwa
mwaka ambayo hutofautiana kati ya mkoa na mkoa.
Katika
kila msimu kazi za mfugaji Nyuki hutegemea kundi la Nyuki linahitaji nini na
mfugaji afanye nini kuweza kuzalisha mazao ya Nyuki.
MSIMU WA NJAA KWA NYUKI
Ni
kipindi cha kiangazi ,ukame na mimea mbalimbali imepukutisha maua na majani.
Matokeo.
·
Chakula kinakuwa kidogo kwenye
mzinga
·
Idadi ya Nyuki hupungua mzingani
·
Malkia hupunguza au huacha kutaga
mayai kabisa.
·
Makundi ya Nyuki kuhama kutafuta
sehemu zenye malisho(ubichi)
·
Baadhi ya makundi ya Nyuki hupita
kwenye kundi lenye asali kuiba.
Wajibu wa Mfugaji Nyuki katika
msimu huu.
·
Chukua tahadhari ya mizinga
usivamiwe na maadui wa nyuki mfano sisimizi,nyegere na wengine wanaotaka
kuingia ndani ya mzinga.
·
Makundi yakingwe kutokana na jua
kali na upepo.
·
Andaa vifaa vya ufugaji
nyuki(kutengeneza mizinga,kukarabati iliyo mibovu)
·
Lisha makundi ya Nyuki imara kwa
asali kama njaa ni kali.
MSIMU WA KUJIJENGA KWA NYUKI.
Hiki
ni kipindi ambapo mvua za awali zimeanza na mimea inachanua kwa wingi.Makundi
ya Nyuki hupita kutafuta makazi pia huzungukazunguka kwenye mzinga na sehemu
nyingine.
Matokeo
·
Nyuki hujenga masega ya asali
·
Nyuki huzaliana kuongeza idadi yao
kwenye mzinga
·
Makundi ya Nyuki hupita kutafuta
makazi
·
Makundi huhama kwenye mizinga endapo
kuna maadui au mzinga kuwa mbovu.
Wajibu wa Mfugaji Nyuki katika
Msimu huu.
·
Fanya ukaguzi wa mizinga na manzuki
kuwa katika hali ya usafi.
·
Safisha na kuambika mizinga isiyo
na Nyuki.
Tafuta
makundi ya Nyuki ili kuwezesha mizinga kuwa na Nyuki kwa njia ya;
Ø Kutundika
mizinga ya kukamatia makundi sehemu ambapo makundi ya Nyuki hupitapita.
Ø Kugawa
makundi makubwa.
Ø Kuzalisha
makundi ya Nyuki.
·
Saidia Nyuki kuongeza kiota kwa
kuweka sanduku la ziada
·
Hakikisha Nyuki wana chakula cha
kutosha
·
Kagua mizinga ya kisasa ya viunzi na
vuna mzinga uliobebeshwa endapo una asali iliyokomaa
·
Tembelea mara kwa mara mizinga yenye
makundi ya Nyuki kuona maendeleo au matatizo.
MSIMU WA MTIRIRIKO WA ASALI KWA
NYUKI.
Ni
kipindi ambapo miti na vichaka vimechanua maua kwa wingi na Nyuki wanatembelea
maua kukusanya mbochi na chavua.Wakati huu ukipita karibu na mimea yenye maua
utasikia sauti za Nyuki.
Matokeo.
·
Nyuki hukusanya mbochi na
kuibadilisha kuwa asali.
·
Maadui wa Nyuki mfano siafu,sisimizi
na wengineo huongezeka jirani na kundi la Nyuki.
·
Nyuki huongezeka kwenye kundi pamoja
na kutengeneza masega.
·
Nyuki hupita kutafuta maji.
·
Weka kumbukumbu za maendeleo ya kila
kundi na manzuki
·
Jenga ushirikiano na wafugaji Nyuki
jirani kwa ajili ya kushughulikia changamoto zinazojitokeza kwa pamoja.
Wajibu wa Mfugaji Nyuki katika
msimu huu.
Ø Fanya
ukaguzi wa mara kwa mara kwenye manzuki na mizinga ya Nyuki.
Ø Fyeka
majani na matawi ambayo yanasonga mizinga ya Nyuki.
Ø Wekea
vizuia wadudu kupanda kwenye mzinga wa
Nyuki wa Nyuki hasa ile inayokaa kwenye vichanja
Ø Weka
masanduku ya ziada kubebesha kwenye mizinga ya viunzi ili kuongeza uzalishaji,
Ø Fanya
maandalizi ya vifaa vya kuvunia na kuhifadhia asali.
Ø Vuna
baadhi ya masanduku yaliyobebeshwa endapo yana asali.
Ø Anza
kutafuta masoko ya Asali unayokadiria kuvuna.
Ø Weka
kumbukumbu za maendeleo ya kila kundi.
MSIMU WA MAVUNO KWA MFUGAJI
NYUKI.
Ni
kipindi ambapo maua ya mimea yamepungua na kuanza kutoa mbegu ama
matunda,kiangazi ndio kinaanza.Sehemu nyingine baada ya kuisha mvua za vuli.Ni
matunda ya kazi ya misimu mitatu iliyotajwa hapo juu na ni jukumu la Mfugaji wa
Nyuki kuvuna mazao ambayo nyuki wamemuandalia.
Matokeo.
·
Nyuki huongeza ulinzi nje ya mzinga
na huwa wakali
·
Baadhi ya mizinga nyuki hujikusanya
nje.
·
Nyuki hupunguza kupitapita kwenye
maua au kuhama.
Wajibu wa Mfugaji Nyuki katika
Msimu huu.
·
Vuna masega yenye asali iliyokamaa.
·
Tumia bomba la moshi,mavazi ya kinga
na vyombo safi wakati wa kuvuna.
·
Bakiza masega kiasi yenye asali
kuwezesha Nyuki kutumia kama akiba.
·
Chuja asali na kuhifadhi katika eneo
sahihi kulingana na ushauri wa kitaalamu.
·
Andaa nta endapo masega yametoka
kwenye mizinga ya miche.
·
Tafuta masoko na kuuza mazao ya
Nyuki.
·
Weka kumbukumbu za mavuno kwa kila
mzinga na manzuki.
·
Toa taarifa zinazohusiana na mavuno
na mauzo ya mazao ya Nyuki kwa Maafisa Ugani waliokaribu.
MABADILIKO YA KALENDA YA
UFUGAJI NYUKI.
Sehemu
ambazo zinapata mvua za vuli na masika kuna kuwa na msimu mdogo wa mavuno na
msimu mkubwa wa mavuno.
Msimu
mdogo wa mavuno huwa ni katika kipindi cha;
Mwezi
Disemba/Januari(siku 14 tu) – Misitu ya miombo.
Mwezi
February(Siku 14 tu) – Vichaka vya nang’ana.
ANGALIZO:
EPUKA KUCHEMSHA ASALI.Asali
iliyokamuliwa vyema na kuhifadhiwa vizuri mahali pasafi bila kuchemshwa huwa
ASALI MBICHI ILIYO BORA.
Kwa maoni/Ushauri niandikie;
fabianbalele@gmail.com
fabianbalele@gmail.com
No comments:
Post a Comment