1) FURSA ILIYOPO TANZANIA JUU YA UFUGAJI WA NYUKI.
2) Maisha ya Nyuki.
3) Nyumba ya Nyuki.
4) Sifa za Eneo linalofaa kwa Ufugaji wa Nyuki.
5) Mavuno.
6) Umuhimu wa Asali
7) Mazao ya Asali
8) Magonjwa yanayotibiwa kwa Asali.
FURSA ILIYOPO TANZANIA JUU YA UFUGAJI WA NYUKI.
Tanzania ina
mazingira mazuri ya kuzalisha mazao ya nyuki kwa kuwa kuna mimea mingi ambayo
inatoa maua yenye kutoa mbochi na chavua vitu ambavyo huwavutia nyuki na
kutengeneza asali.
Katika Tanzania mazao makuu yatokanayo na ufugaji wa nyuki ni
asali na nta. Hata hivyo kuna mazao mengi
ambayo yanaweza kuzalishwa kutokana na asali na nta.
Tanzania tumejaliwa maeneo mengi sana na makubwa
yenye misitu minene yenye chavua na nectar kwa wingi, maeneo haya yapo karibu
Tanzania nzima hayana matumizi yoyote yale ya ufugaji wa nyuki, kwa nchi nyingi
Africa kama vile Ethiopia na nchi nyinginezo ambazo zinasemekana kuongoza kwa
ufugaji nyuki zinatamani sana maeneo mazuri tuliyonayo.
Ukizunguka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Tabora,
Rukwa, Katavi, Kigoma, Singida,Dodoma, Shinyanga na Mikoa mingine mingi,
rasilimali hizi za misitu zimebweteka na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa na
serikali yetu ya kuwekea mkazo katika kuwekeza kwa ufugaji wa nyuki.
Tusisitize serikali za vijiji kutoa maeneo hayo
ya misitu yenye mahitaji ya nyuki kwa vikundi mbalimbali vya wafugaji nyuki ili
kuweza kuiboresha na kuiendeleza idara hii ya ufugaji nyuki
Maisha ya Nyuki
Nyuki ni mdudu mwenye mabawa manne angavu na mwiba nyuma ya mwili wake anayekusanya mbelewele ya maua kama chakula
chake. Aina inayojulikana hasa ni nyuki wa asali wa familia apis. Kuna
spishi zaidi za 20,000 zinazojumlishwa na biolojia kati ya nyuki lakini ni wale
wa jenasi apis wanaokusanya asali inayovunwa na wanadamu.
Nyuki za asali mara nyingi wanafugwa lakini wengine wanaishi porini na asali yao inakusanywa kwa kuvunja mzinga wao. Katika Afrika kwa jumla sehemu ya asali bado inatokana na nyuki asali wa porini lakini ufugaji nyuki unapanua.
Hapo mwanzo Wanajamii walikuwa wanafuga nyuki kwenye magome ya miti, vibuyu, vyungu, mapango, vichuguu na kwenye miamba. Baada ya muda ufugaji ulipiga hatua kidogo na watu wengi wakawa wanafuga kwa kutumia mizinga iliyochongwa kutoka kwenye magogo ya miti. Ufugaji wa aina hii umedumu kwa karne nyingi kote nchini Tanzania.
Kutokana
na uhitaji na ongezeko la matumizi ya bidhaa za nyuki, kulifanyika tafiti
mbalimbali ambazo ziliweza kuboresha ufugaji wa nyuki kwa kuwa na mizinga ya
kisasa ambayo imewezesha uzalishaji wa asali kuwa mkubwa na kuongeza pato la
wafugaji tofauti na ilivyokuwa hapo awali. Tafiti hazikuishia kwenye kuboresha
mizinga tu, ila siku hadi siku kunavumbuliwa namna bora zaidi za kuimarisha
uzalishaji wa nyuki.
Nyumba ya nyuki.
Hii
ni aina mpya ya ufugaji wa nyuki ambapo unaweza kujenga kibanda au nyumba kisha
kuweka mizinga idadi unayohitaji.
Ni kwa nini kujenga nyumba au kibanda?
Ø Ni muhimu kufuga nyuki
kwenye kibanda au kwenye nyumba kwa sababu inasaidia kudhibiti wizi wa mizinga,
pamoja na wanyama wanaokula asali na kudhuru nyuki.
Ø Inarahisisha utunzaji wa
mizinga na kuwafanya nyuki wasihame kwenda sehemu nyingine.
Ø Inasaidia watu wengi
kujifunza namna nzuri ya ufugaji wa nyuki, ikiwa ni pamoja na watoto, jambo
ambalo linafanya shughuli hii kuwa endelevu.
Ø Ufugaji wa aina hii
unasaidia kuwakinga nyuki dhidi ya majanga kama vile moto, na mafuriko.
Ø Inawaepusha nyuki na
usumbufu unaoweza kuwafanya wasizalishe kwa kiwango kinachotakiwa.
Ø
Uzalishaji unaongezeka. Hii ni kwa sababu mizinga inayotumika ni ile
ya kibiashara. Mzinga 1 unapata asali kilo 30 sawa na lita 20.
Aina ya nyumba
Unaweza
kujenga nyumba yenye upana wa futi 3 na urefu wa futi 9. Nyumba hii inaweza
kuchukua mizinga hamsini. Halikadhalika, unaweza kujenga kibanda chenye ukubwa
sawa na huo.
PICHA ZA MABANDA TOFAUTI TOFAUTI YA KUFUGIA NYUKI
SIFA
ZIFAAZO KWA MAENEO YA KUFUGIA NYUKI (MANZUKI)
Eneo
lifaalo kwa shughuli za ufugaji nyuki ni lazima liwe na sifa zifuatazo:
Ø (i)
Miti, uoto wowote wa asili na mimea mbalimbali kwa mfano mazao ya chakula na
biashara, Kusiwe
na aina ya mimea ambayo nyuki hawapendi.
(ii)
Maji ya kudumu ambayo hutumika kama sehemu ya chakula cha jamii nzima ya kundi
la nyuki. Pia maji hutumika kwa kurekebisha hali ya hewa ndani ya mzinga.
Ø (iii)
Eneo la shamba la nyuki ni lazima liwe ni salama kwa mizinga, mazao yake,
mifugo, binadamu, na mahali ambapo maadui wa nyuki hawapo au wanaweza
kudhibitiwa(Ili
kuwa na ufanisi mzuri, nyumba hii inafaa kujengwa nje kidogo ya makazi ya watu,
Kusiwe na mifugo karibu, Iwe sehemu ambayo watoto hawawezi kufika, Isiwe karibu
na njia ambayo watu wanapita mara kwa mara.)
(iv)
Kivuli cha kadri na kinga ya upepo ili kuwapunguzia nyuki kazi kubwa ya ubebaji
maji kwa ajili ya kupunguza joto. Inafaa kufugia nyuki ndani ya nyumba
iliyoandaliwa kwa ajili ya ufugaji wa nyuki(bee-house)
Mawasiliano
ya barabara ni muhimu yawepo ili kurahisisha uhudumiaji wa makundi ya nyuki
pamoja na mazao yake hadi kufikia sokoni.
Mavuno
Baada
ya kujenga nyumba, kuweka mizinga na nyuki kuingia, unaweza kuvuna kwa mara ya
kwanza baada ya miezi mitatu. Utaweza kupata mavuno mazuri endapo utavuna kabla
nyuki na wadudu wengine hawajaanza kula asali.
Ni
muhimu kuhakikisha kuwa wadudu waharibifu kama vile sisimizi, mende na wengineo
wanadhibitiwa ili kutokuathiri uzalishaji wa asali. Hakikisha unavuna kitaalamu
ili kuepuka upotevu wa asali. Endapo nyuki
wametunzwa vizuri na kwenye mazingira mazuri, unaweza kuvuna asali mara tatu
kwa mwaka. Katika mzinga mpya nyuki wana uwezo wa kutengeneza masega kwa siku
tatu na kuanza uzalishaji wa asali.
Ni nini umuhimu wa asali
•
Asali inatumika kama chakula
•
Inatumika kama tiba ya magonjwa mbalimbali
•
Hutumika kutibu majeraha
•
Ni chanzo kizuri cha kipato
•
Hutumika katika kutengeneza dawa za binadamu
*Asali
inaweza kuhifadhiwa kwa miaka mingi sana bila kuharibika. Hii inatokana na
wingi wa dawa maalum iliyo nayo inayofanya isiharibike.
MAGONJWA YANAYOTIBIWA KWA
MATUMIZZI YA ASALI.
1. Ugonjwa wa
viungo/maumivu na uvimbe.
2. Kukatika kwa
nywele.
3. Ukungu wa
miguu.
4. Maambukizo
kwenye kibofu cha mkojo.
5. Maumivu ya
jino.
6. Helemu
(Cholestral).
7. Ugumba
8. Mchafuko wa
tumbo.
9. Ugonjwa wa
moyo
10. Shinikizo
la damu.
11. Kinga ya
mwili.
12. Ukosefu wa
nguvu za kiumbe.
13. Flu.
14. Umri wa
kuishi.
15. Chunusi.
16. Kuumwa na
wadudu (kwa washawasha) wenye sumu.
17. Madhara ya
ngozi.
18. Kupungua
kwa uzito.
19. Saratani.
20. Uchovu
mwilini.
22. Harufu
mwilini.
23. Kupungua kwa usikivu.
Bidhaa zinazotokana na asali
Kuna aina nyingi ya bidhaa zinatokana na asali, kwa
kutengenezwa na nyuki wenyewe na nyingine zikitengenezwa na binadamu
kutokana na tafiti mbalimbali. Miongoni mwa bidhaa hizo ni:
• Asali yenyewe
• Royal jelly :
Hii ni aina ya maziwa yanayotengenezwa na nyuki, ambayo hutumika kama tiba.
•
Gundi: Hii hutumika kutengeneza bidhaa za aina
mbalimbali kulingana na mahitaji ya mtumiaji.
•
Nta: hutumika kutengenezea mishu maa, kulainisha
nyuzi, kutengeneza dawa ya viatu, mafuta ya kupaka, pamoja na dawa ya ngozi.
SHAMBA LA NYUKI.
SHAMBA LA NYUKI.
MZINGA WA KISASA WA NYUKI
KWA USHAURI NA MAONI.
NIANDIKIE:fabianbalele@gmail.com
+255768937884
Exclusive to: balelemwanahabari.blogspot.com
asante sana
ReplyDelete