Wakikiongea katika kipindi maalumu cha VIJANA ktk mada ya Jinsi ufugaji wa nyuki unavyoweza kumkomboa kijana wa kitanzania kinachorushwa kila J'mosi SUA-TV vijana Kutoka Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine(SUA)-Morogoro wanaosoma shahada ya kwanza ya Misitu walithibitisha kua ufugaji wa nyuki ni njia ya haraka zaidi ya kujipatia utajiri wa HALALI.
Wkiongea katika kipindi hicho kilichoandaliwa na Tanzania Forestry Students' Association(TFSA),Wanafunzi hao walithibitisha kua Mzinga mmoja kwa wastani unauwezo wa kuzalisha asalli lita 10,kwa bei ya lita 1 sawa na sh.10,000 iwapo utakua na mizinga 20 basi utapata kiasi cha Tsh.Milioni 2,kiasi ambacho kinaweza kumkwamua kijana kutoka ktk wimbi la umasikini.
Ufugaji wa nyuki ni shughuli rahisi isiyohitaji mtaji mkubwa kama zilivyo shughuli nyingine.
Asali hutumika kama chakula,dawa za binadamu, losheni,kuokea mikate,kukoleza tumbaku na matumizi mengineyo.
Mbali na asali nyuki pia wanazalisha inta amabayo inatumika kutengeneza bidhaa mbalimbali kama vile dawa za kulainisha ngozi,mishumaa,karatasi za kaboni na creams mbalimbali za urembo.
Tanzania ni mojawapo ya nchi Tano za Afrika zilizoruhusiwa kuuza asali yake katika soko la nje hasa la umoja wa nchi za Ulaya.
Nchi inayoongoza Afrika kwa uzalishaji wa asali ni Ethiopia.
Nchi nyingine zilizoruhusiwa kuuza asali ktk soko hilo ni Ehiopia,Uganda,Zambia na Madagascar.
Inakadiriwa kua iwapo Ufugaji wa nyuki utapewa kipaumbele,Tanzania ina uwezo wa kuzalisha Tani 138,000 za asali kwa mwaka zenye thamani ya Bilioni 133.3.Pia inaweza kuzalisha tani 9200 za inta zenye thamani sawa na 35.5 bilion kwa mwaka.
Kwa sasa Tanzania iazalisha tani 4860 pekee za asali zenye thamani ya Sh.4.9 Bilioni na inta tani 324 sawa na 648 Milioni kwa mwaka
.
Wanunuzi wakubwa wa asali ya hapa nchini ni Kenya,Ujerumani,Uingereza,Uholanzi,Ubelgiji,Hispania na Italia.
Wanunuzi wakubwa wa inta ya Tanzania ni Japani,Uholanzi,Marekani,Ujerumani na Ufaransa.
Soko la ndani la asali ni 10,000 mpaka 20,000/= kwa lita moja,Ambapo soko la nje ni wastani wa dola 4.5 kwa lita.
Tanzania kuna takribani wilaya 30 zinazohusika na ufugaji wa nyuki.
Baadhi ya wilaya hizo ni Manyoni,urambo,Lindi,Songea,Sikonge, na Chunya
Serikali ya Tanzania tayari imeandaa sera na mikakati kuhakikisha kua ufugaji wa nyuki unakua endelevu.Hii ni pamoja na kuanzisha upya chuo kinachotoa Astashahada na Stashahada za elimu ya nyuki kilichopo Tabora.
Serikali pia kwa miaka 2011/2012 na 2012/2013 imekua ikifadhili mizinga 5000 kila mwaka ktk baadhi ya wilaya hizi 30.
Mizengo Pinda Waziri Mkuu wa Tanzania ni Mdau mkubwa wa Ufugaji wa nyuki huko Katavi..
Somo la nyuki pia hufundishwa katika chuo kikuu cha Sokoine Kilichopo Morogoro.
Endapo utahitaji msaada wowote jinsi ya Kuanzisha Ufugaji wa nyuki Tuwasiliane kupitia
KULIA:Wanafunzi wa shahada ya kwanza ya Misitu Chuo kikuu cha Sokoine Morogoro wakishiriki mjadala ktk kituo cha televisheni cha Sua Tv Katika mada ya Ufugaji wa Nyuki unavyoweza kumkomboa Kijana iliyoandaliwa na TFSA(Tanzania Forestry Students' Association)
Fabian Frank Balele akibainisha changamoto za ufugaji wa nyuki katika mada hiyo.Ambapo miongoni mwa changamoto kubwa ni utayari wa vijana kujihusisha katika ufugajai wa nyuki,shughuli ambayo imekua haitiliwi maanai na vijana walio wengi kwa kupenda kazi za maofisini pekee.
Kundi kubwa la nyuki likiwa limejikusanya kwenye majani ya nyuki,Nyuki hawa wakiandaliwa mazingira ya ufugaji wanaweza kua chanzo kizuri cha ufugaji wa nyuki.Inakadiriwa kua kundi moja la nyuki lina uwezo wa kua na nyuki hadi 80,000 Ambapo Malkia hua ni mmoja tu ktk kundi hilo.
Mizinga ya Kienyeji ya Nyuki,Mizinga hii ndimo hutumiwa kama nyumba ya nyuki katika ufugaji.
Asali nyingi ya Afrika inatokana na Mizinga ya Kienyeji kutoka na ile ya kisasa kua na bei ghali hadi kufikia 70,000/= kwa mzinga mmoja.
Mizengo Pinda Waziri Mkuu wa Tanzania akiweka jiwe la msingi katika mradi mpya wa ufugaji wa nyuki Mkoani Geita Kijiji cha Bugulula.
Kwa mbele ni Mizinga ya nyuki ya kisasa kwa ufugaji wa nyuki wa kisasa.
Mizengo Pinda akifungua jiwe la Msingi ktk Mradi wa Nyuki ulioko Kwimba Mkoani Mwanza.
Kwa nyuma kushoto ni mkewe Mama Tunu Pinda,Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarest Ndikilo.
Mizengo Pinda ni Mdau Mkubwa wa Ufugaji WA Nyuki Tanzania Nyumbani kwake Katavi.
Mazao ya Nyuki, Asali.
Chini kushoto ni Lotion Itokanayo na Inta ya nyuki.
ASALI
No comments:
Post a Comment