Monday, December 31, 2012

MATUKIO MUHIMU 2012

Mwaka 2012 umekua mwaka  wa kihistoria kwa namna yake kutokana na matukio mbalimbali ya kisiasa,kijamii na kiuchumi kwa hapa Tanzania  na Duniani kwa ujumla.
Kwa hapa Tanzania matukio yafuatayo yalionekana kupewa nafasi ya kipekee.

1)KIFO CHA MSAANI NGULI WA FILAMU-STEVEN CHARLES KANUMBA.
Si tu kwa watu wakubwa bali hata kwa watoto wadogo,tukio la kifo cha msanii nguli wa Tasnia ya Filamu nchini na Afrika ya Mshariki hadi Afrika ya Kati kilionekana kuwahuzunisha walio wengi.
Steven Kanumba aliitangaza nchi ya Tanzania nchi za nje hasa Afrika Mshariki,Afrika ya kati na Afrika Mgharibi kupitia Tasnia ya Filamu,
Miongoni mwa filamu alizowahi kuigiza ni pamoja na THIS IS IT,UNCLE JJ,THE BIG DADDY,DEVEL KINGDOM,MOSES,BECAUSE OF YOU,YOUNGER MILLIONAIRE,THE SHOCK,DECEPTION,KIJIJI CHA TAMBUA HAKI
Steven Kanumba alizaliwa 8/1/1984 na kufariki   usiku wa Tarehe 6/4/2012








  Bi.Flora, Mama mzazi wa Kanumba.












2)KUZAMA KWA MELI YA MV.SKAGIT

Ni tukio lililoacha majonzi makubwa kwa Watanzania wa Bara na Zanzibar kwa Ujumla
Ilikua ni tarehe 18/7/2012 Meli ijulikanayo kwa jina la Mv.Skagit ya kampuni ya SEAGULL ilpozama eneo la Chumbe ikiwa na Abiria 250.
Abiria waapatao 150 waliokolewa ktk ajali hiyo.
Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo wakisubiri kuokolewa wakiwa kwenye mgongo wa meli hiyo.

    Askari wakiwa wamebeba maiti ya mmoja wa watu waliokufa ktk ajali hiyo


   HEKA HEKA ZA UBUNGE WA LEMA
Mwaka 2012 pia katika duru za kisiasa nchini Tanzania utakumbukwa kwa hekaheka za za kuvuliwa ubunge wa Godbless Lema Mbunge wa Arusha Mjini.
Jaji Mfawidhi Gabriel Rwakibarika wa Mahakama ya kanda ya Sumbawanga alimvua ubunge Lema April 5 2012.

Kesi ya Kupinga matokeo ya ushindi wa Ubunge wa Arusha mjini dhidi ya mgombea wa CCM Dr. Batilda Burian ilifunguliwa na makada wa CCM Hapiness Kivuyo,Agnes Molel na Musa Mkenga. kwa kupinga kua Lema alitumia lugha ya matusi dhidi ya Dk. Buriani kipindi cha Kampeni.

Hata hivyo Mahakama ya rufaa ilimrejesha Lema kua Mbunge halali wa Arusha Mjini baada ya Kushinda rufaa ya kesi hiyo tarehe  21 Dec 2012. 
Godbless Lema na wafuasi wa CHADEMA mara baada ya hukumu ya kupinga Ubunge wake kutolewa kua si Mbunge Halali wa Arusha mjini ktk mahakama kuu kanda ya Arusha.
 Godbless Lema na wafuasi wa CHADEMA baada ya ushindi wa rufaa yake katika makama ya rufaa jijini Dar es Salaam

KUTEKWA NYARA KWA DK. ULIMBOKA
Mwaka 2012 pia utakumbukwa kwa tukio la  mgomo wa madaktari hali iliyopelekea kupoteza maisha kwa baadhi ya wagonjwa.

Tukio kubwa ktk hekeheka za mgomo wa madaktari pia ni kutekwa nyara kwa mwenyekiti wa jumuiya ya madaktari Dk. Steven Ulimboka.

Dk. Steven Ulimboka ndiye aliyekua kiongozi wa madaktari aliyekua akiratibu suala zima la kuidai serikali itekeleze malalamiko ya madaktari ikiwemo mazingira mazuri ya kufanyia kazi,kuwepo kwa vifaa vya matibabu,posho mbalimbali kama posho ya usafiri,kufanya kazi ktk mazingira magumu.

Mdaktari pia waliitaka serikali kuwapatia Green Card za bima ya afya,kuwaondoa watendaji wakuu ktk wizara ya afya akiwemo waziri wa afya,katibu mkuu wa wizara hiyo na Mganga mkuu wa serikali.

Serikali ilitimiza baadhi ya mahitaji hayo ikiwepo kuwapatia Green card za bima ya afya,kuawaondoa waziri,katibu mkuu na Mganga mkuu wa Serikali  na mambo mengine.

Katika hali isiyo ya kawaida  Dk. Ulimboka alitekwa na watu wasiojulikana kisha kuteswa kwa kung'olewa kucha,meno na kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake kisha kutupwa katika msitu wa Magwepande ulio nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.  
Dk. Steven Ulimboka akiwa amefikishwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuokotwa na msamaria mwema ktk msitu wa Magwepande.

      Dk. Ulimboka akiendelea kupata matibabu ktk hospitali ya Taifa ya Muhimbili.hata ivyo Dk. Ulimboka alihamishiwa Afrika ya kusini kwa matibabu zaidi baada ya hali yake kubadirika.
Dk. Ulimboka katika moja ya vikao akijaribu kuonyesha msisitizo kua Serikali inapaswa kuzingatia malalamiko ya madaktari nchini.


KIFO CHA MWANDISHI WA HABARI-CHANEL TEN-DAUD MWANGOSI
Hili pia ni tukio kubwa lililoacha majonzi na simanzi kubwa miongoni mwa Watanzania.
Daudi Mwangosi aliyekuwa mwakilishi wa kituo cha utangazaji chanel ten alifariki alipokua akitekeleza majukumu yake ya kikiazi ya uandishi huko Mkoani Iringa - kijiji cha Nyororo ambapo inadaiwa kua CHADEMA kilikua kikifanya shughuli zake zakisiasa katika harakati zao za M4C.

Kufuatia kifo hicho tume mbalimbali ziliundwa kuchunguza mazingira tatanishi ya kifo chake kutokana na uvumi kua alilipuliwa na bomu la machozi,huku wengine wakidai kua alipigwa na kitu kizito kichwani.

Tume zilizoundwa ni pamoja na ile ya Mh. Nchimbi waziri wa mambo ya ndani ya Nchi pamoja na ile iliyoundwa na chama cha waandishi wa habari.

                                                      Daud Mwangosi Enzi za uhai wake

.
                  KIFO CHA MCHEZAJI WA MPIRA-PATRICK MAFISANGO
Mwaka 2012 utakumbukwa pia kwa tukio la kusikitisha la ajali  Iiyosababisha kifo cha mchezaji wa Timu ya SIMBA Patrick Mafisango.


 
Patrick Mafisango enzi za uhai wake akiwajibika ipasavyo uwanjani katika moja ya mechi za timu ya Simba.













Gari aliyokua nayo Mafisango ikiwa imeharibika vibaya baada ya ajali hiyo kutokea.






wacezaji wa SIMBA pamoja na waombolezaji wengine wakiuaga mwili wa Mafisango.









KUANZISHWA KWA TUME YA KUKUSANYA MAONI YA KUAANDAA RASIMU YA KATIBA MPYA TANZANIA.
Kuanzishwa kwa tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya Hapa Tanzania ni moja ya tukio muhimu la kukumbukwa hapa Tanzania.
Tume hii ilianzishwa rasimi na Mh. KIKWETE Raisi wa Tanzania kwa mujibu wa Katiba ya sasa.
Tume ilipewa miezi 18 kukamilisha zoezi hilo.
Kuna mategemeo makubwa ya kutumia Katiba Mpya Katika Uchaguzi ujao wa mwaka 2015.





Kushoto:Mwenyekiti wa Tume ya mabadiriko ya katiba Jaji mstaafu (Jaji Warioba) akiwa na viongozi na wanachama wa CUF walipofika ktk ofisi za Tume Hiyo Kuwasilisha Maoni ya Chama hicho.





KIFO CHA SHARO MILLIONAIRE.
2012 Utakumbukwa kwa majonzi baada ya kumpoteza Msanii wa maigizo Sharo Miliionaire Aliyefariki baada ya kupata ajali akielekea nyumbani kwao Mkoani Tanga.
                                                   Sharo Millionaire enzi za Uhai wake.



                                      UVUMI WA MIKE-TYSON KUBADILI JINSIA
Mwishoni mwa mwezi November mwaka jana 2012,Kulitokea uvumi mkubwa katika vyombo mbalimbali kua Mike Tyson Bondia wa Zamani wa Uzito wa Juu DUNIANI alibadili jinsia.
Hata ivyo uvumi huo ulikanushwa na Mike Tyson Mwenyewe kama ilivyoripotiwa na shirika la Utangazaji la BBC.

No comments:

Post a Comment