Tuesday, January 15, 2013

TRAFFIC UBUNGO TAFUTENI UFUMBUZI WA TATIZO HILI.

Tunamshukuru sana waziri wa Mawasiliano na uchukuzi Mh. Dk. Harryson Mwakyembe kwa juhudi kubwa anazozifanya kuhakikisha kuwa anawajibika ipasavyo ktk wizara yake ili kurahisisha shughuli za kimaendeleo za wananchi  wa Tanzania.

Waziri  Mwakyembe amekua mstari wa mbele kuhakikisha kua sekta ya uchukuzi inafanya kila juhudi ili kuatoa  huduma bora za uchukuzi
.
Kwa kuzingatia hilo Waziri Mwakyembe amekua akifanya ziara za kushtukiza Stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani ya Ubungo Jijini Dar es Salaam ili kujionea hali halisi ya huduma za usafiri mahali hapo.

Jambo kubwa ambalo amekua akilisisitizia ni kuhakikisha kua Abiria wanatozwa pesa za nauli stahili kulingana na safari husika na si vinginevyo.

Jambo lingine ni kuhakikisha kua Mabasi hayo yanakidhi vigezo mbalimbal vya safari ndefu .

Hata hivyo Askari wa barabarani wamekua wakiendesha zoezi hilo kwa kutumia mda mwingi sana kiasi cha kusababisha adha kubwa kwa abiria hasa waendao mikoani kutokana na kukaa ndani ya basi mda mrefu wakisubiri mabasi hayo kukaguliwa hasa nyakati za asubuhi..

Tunapenda kuwashauri Askari hao kubuni njia rahisi ya kukamilisha zoezi hilo kwa haraka zaidi ili kuepusha msururu mkubwa wa mabasi yaendayo mikoani hapo UBUNGO.

BAADHI YA MABASI YENDAYO MIKOANI YAKISUBIRI KUKAGULIWA NA ASKARI WA KIKOSI CHA BARABARANI-TRAFFIC katika Stand ya Mabasi ya UBUNGO Jijini Dar es Salaam kama yalivyokutwa na Balele Mwanahabari.

No comments:

Post a Comment