Thursday, January 17, 2013

ASASI ISIYO YA KESERIKALI(NON GOVERNMENTAL ORGANIZATION-NGO's)IITWAYO EXPERT'S ALLIANCE FOR COMMUNITY EMPOWERMENT-EACE YAANZISHWA.

     HONGERA KWA KUKAMILISHA       USAJILI.............
 Bwn. Fabian Balele Katibu Mtendaji wa EACE Akikabidhiwa Cheti cha Usajili wa Asasi isiyo ya Kiserikali iitwayo EXPERT'S ALLIANCE FOR COMMUNITY EMPOWERMENT-Makao makuu ya Ofisi za Wizara ya Maendeleo Ya Jamii Jinsia Na Watoto Jijini Dar es Salaam.

EXPERT'S ALLIANCE FOR COMMUNITY EMPOWERMENT(EACE) Ni Asasi isiyokua ya kiserikali inayodhamiria  kuiwezesha jamii ya Kitanzania kwa kurahisisha upatikanaji wa huduma za Elimu Bora,Afya,msaada wa Kisheria,kuanzisha miradi mbalimbali,kupunguza maambukizi ya ukimwi,kujenga fursa za ajira,kuwawezesha wahitimu mbalimbali katika vyuo hapa nchini kupata ajira na huduma nyinginezo ili kupunguza umasikini na kuisaidia serikali katika kutekeleza sera mbalimbali zinazolenga kuisaidia jamii ya kitanzania.

EACE Ni Asasi inayowaunganisha wanafunzi mbalimbali wa vyuo vikuu hapa Tanzania wenye nia ya kuisaidia Jamii ya Kitanzania kwa kutumia Elimu,Ujuzi na Maarifa wanayoyapata kipindi cha masomo yao.

Akiongea kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Morogoro, Katibu Mtendaji wa Asasi hiyo Bwn. Fabian Balele  ameeleza kua mchakato mzima wa Usajili wa Asasi Hiyo umekwishakamilika ambapo Asasi ilisajiriwa Rasmi tarehe 03 JAN 2013 Makao makuu ya wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na watoto Jijini Dar-es-Salaam.

Alizidi kubainmisha kua Asasi hiyo imeanzishwa na wanachama 12 kutoka vyuo mbalimbali hapa Tanzania kama vile SUA,IFM,UDOM,CUHAS-BUGANDO,ARDHI.
Baada ya usajili mchakato wa kuwapata washiriki wengine kutoka vyuo mbalimbali unafanyika.
Kwa sasa Mchakato wa kupata FUNDS kwa ajili ya OFFICE unafanyika,kama ilivyobainishwa na Mwenyekiti wa Asasi iyo Bwn. Fransisi Msonge.
Afisa wa Usajili wa NGO's Wizara Ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Na Watoto Akiandaa Documents Muhimu tayari kwa  kumkabidhi Katibu Mtendaji wa EACE Bwn Fabian Balele Baada ya Kukamilisha Taratibu Za usajili Wizarani Hapo.

Makao makuu ya Asasi hiyo ni Jijini Mwanza.
Waweza kuwasiliana nao kupitia.

Email address, eacetanzania@gmail.com
Mobile no.   +255757979629- Chair  Person.

                      +255768937884-The Executive secretary
                       +255762446463-Treasury.

No comments:

Post a Comment