Akieleza kwa masikitiko makubwa Rais wa Serikali ya wanafunzi Chuo kikuu cha Sokoine- SUA Bwn, IDD IDD,alieleza kua kifo cha Marehemu Ryoba Munchari kilitokea ghafla," Marehemu aliugua ghafla usiku huo na kukimbizwa hospitali ya chuo na mda mfupi baada ya kufikishwa hospitali akawa amekata roho."
Inasemekana kua mda mfupi kabla ya kifo chake Marehemu alikua ktk msongo wa mawazo baada ya mjane wa marehemu kujifungua kwa operation,paka kifo kinamkuta mjane wa marehemu alikua amelazwa hospitalini kutokana na kujifungua kwa operation.
Mwili wa Marehemu uliagwa rasmi tarehe 7/12/2012 mchana ktk ukumbi wa Freedom Square-SUA,na mda mfupi baada ya IBADA maalumu ya kumuombea Marehemu,mwili ulisafirishwa kuelekea mkoani Mara kwa ajili ya mazishi.
Marehemu alikua mwajiriwa wa shule ya sekondari LAMADI Mkoa wa SIMIYU na mwaka 2010 ndipo marehemu alipoanza masomo ya Shahada ya kwanza ya Ualimu.
Marehemu ameacha mjane na mtoto mmoja.
"BWANA ALITOA, BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE"
MAJAMBAZI WAVAMIA GARI LA WASINDIKIZAJI WA MWILI WA MAREHEMU
Katika hali isiyo ya kawaida Watu wanaosadikika kua majambazi wakiwa na bunduki aina ya Gobore na siraha nyingine za jadi walivamia gari lililokua likisindikiza mwili wa marehemu usiku wa tarehe 8/12/2012 Majira ya sa 7:30 kilomita chache kabla ya kuingia mjini Singida.
Akiongea kwa masikitiko makubwa Raisi wa serikali ya wanafunzi-SUA Bwn IDD IDD ambaye pia alikua katika msafara aldai baada ya kufika eneo la tukio walikuta mawe makubwa yamepangwa njiani na ndipo walipoamriwa kushuka nje na kuacha kila kitu walicho kua nacho,majambazi hayo yalifanikiwa kuchukua fedha zote walizokua nazo,mabegi ya nguo,simu,computer ndogo(laptop)pamoja na vitu vingine walivyokua navyo
.
Vili vilie wasindikaizaji hao walijeruhiwa sehemu mbalimbali kupelekea kufikishwa katika hospitali ya mkoa-SINGIDA kwa ajili ya matibabu
.
Kama hiyo haitoshi, majambazi hayo yalibomoa jeneza alimokua amehifadhiwa maiti kwa kudhani kua kutakua na pesa iliyo kua imeficha humo.
Baada ya tukio hilo mawasiliano yalifanyika na gari nyingine ilitumwa kutoka SUA kwa ajili ya kuendelwa na safari ya kuasafirisha mwili wa marehemu Ryoba Munchari.
GARI YA MSALABA MWEKUNDU IKIWASILI KTK UKUMBI WA FREEDOM SQUARE-SUA NA MWILI WA MAREHEMU RYOBA MUNCHARI TAYARI KWA KUANZA IBADA YA KUMUOMBEA MAREHEMU.
WANAFUNZI WA SUA WAKIWA WAMEJIANDAA KULIPOKEA JENEZA LA MAREHEMU
MUOMBOLEZAJI AKIWA NA PICHA YA MAREHEMU RYOBA MUNCHARI
JENEZA LENYE MWILI WA MAREHEMU RYOBA MUNCHARI LIKIWA MBELE YA UKUMBI WA FREEDOM SQUARE TAYARI KWA IBADA MAALUMU YA KUUAGA MWILI |
No comments:
Post a Comment