Friday, December 21, 2012

LEMA MBUNGE HALALI WA ARUSHA MJINI.

Mahakama ya rufaa Tanzania imemthibitisha Godbless Lema kua ni Mbunge halalai wa Arusha Mjini baada ya kushinda rufani kufuatia kesi iliyofunguliwa dhidi yake ya kupinga ushindi wa ubunge wake kwa tuhuma kua alitumia lugha ya matusi na ubaguzi wa kijinsia katika moja ya mikutano yake wakati wa kampeni dhidi ya mpinzani wake Dk.Batilda Burian wa CCM.
.
 Akiongea kutoka ktk ofisi za Mahakama ya Rufaa Mh.Tundu Lisu ambae ni Mkurugenzi wa Haki na Sheria wa CHADEMA alidai kua malalamiko hayo ni batili kwa kua mawakili wa mlalamikaji wameshindwa kuthibitisha kua:

 1)Ni kwa jinsi gani mshtakiwa alitumia lugha ya matusi Na udhalilishaji wa kijinsia. 
2)Ni kwa jinsi gani lugha ya matusi iliwaathiri wapiga kura kupelekea kushawishika kutompigia kura Dr. Buriani,
Vilevile Alidai kua walalamikaji hawakuthibitisha kama walikua ni wapiga kura au wenye sifa za kupiga kura hivyo hawakua na sifa kisheria kufungua kesi hiyo.

 Godbless Lema alivuliwa ubunge wa Arusha mjini na Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha April 5 mwaka huu chini ya Jaji Gabriel Rwakibarila kufuatia tuhuma za walalamikaji,Musa Mkenga,Agnes Mollel na Hapiness Kivuyo,Waliofungua mashtaka mahakamani kupinga ushindi wa Godbless Lema kwa kua Alitumia lugha ya matusi na Uzalilishaji wa kijinsia. 

 Baada ya ushindi wa rufani hiyo Mahakama ya Rufaa imemtangaza Godblee Lema kua ni Mbunge Halali wa Arusha Mjini kupitia CHADEMA.  

 Makada wa CCM(Hapiness Kivuyo,Agnes Molel na Mussa Mkenga ) Waliofungua mashtaka ya kupinga ushindi wa Lema
Godbless Lema na wafuasi,viongozi wa CHADEMA wakishangilia ushindi wa rufani hiyo.

No comments:

Post a Comment