Takribani wiki 2 zilizopita sasa kumekuwepo na uvumi wa yule aliyekua Bondia wa uzito wa juu Duniani Mike Tyson kua amebadili jinsia na ataitwa Michelle.
Inadaiwa kua uvumi huo si wa kweli na habari za kukanusha uvumi huo zimethibitishwa na Mike Tyson mwenyewe na kuripotiwa na Shirika la utangazaji la BBC.
Inasemekana kua uvumi wa Mike Tyson kubadili jinsia ulianzia kwenye website ya Satritical ya NewsBiscuit iliyoko inhini Uingereza mwishoni mwa mwezi November
Website ya NewsBiscuit handika makala mbalimbali za kubuni zisizo za ukweli na kuwahi kutokea.
Kwa kasi kubwa uvumi ulichochewa zaidi na makala mbalimbali za Afrika kwa kuanzia gazeti kubwa nchini Zimbabwe la The Standard kisha kuendelea ktk website ya SpyGhana.
Kwa hapa Tanzania habari hiyo iliripotiwa na magazeti mbalimbali makubwa.
.
Kwa bahati mbaya zaidi Watanzania wengi wameendelea kudanganywa kua jambo hilo ni la ukweli huku magazeti mbalimbali yakiendelea kuripoti kua Sasa Mike Tyson ataitwa Michelle na tayari amepata Bwana.
No comments:
Post a Comment