Friday, August 2, 2013

MAONI KUHUSU RASIMU YA KATIBA MPYA,YALENGE MASLAHI YA TAIFA LETU.







 Makamu wa Raisi Mh,Ghalib Bilal akionyesha ishara ya uzinduzi wa Rasimu ya Katiba Mpya.Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiriko ya Katiba Jaji Msaafu Joseph Warioba na Kushoto kwake ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda.

 1/8/2013
 NAIPENDA NCHI YANGU
 By Fabian Balele(Mwananchi Mzalendo)
Mchakato wa Upatikanaji wa katiba Mpya nchini unaendelea  huku kukiwa na Mijadala mbalimbali inayofanyika miongoni mwa Taasisi,mashirika Binafsi,vyama vya siasa na Wadau mbalimbali.
Kumekua na Maoni mbalimbali miongoni mwa Wachangiaji kuhusu vipengele Mbalimbali kama vilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiriko ya Katiba Nchini, Chini ya Jaji Mstaafu,Joseph Warioba.
Miongoni mwa Vipengele vilivyoshika nafasi ya Juu katika uchangiaji wa Rasimu ya Katiba Mpya ni Pamoja na Muundo wa Serikali tatu,Umri wa Mgombea Uraisi,Maadili ya Viongozi wa Uma na Haki za Raia.
Kumekua na mvutano mkali juu ya Muundo wa Serikali tatu hasa katika vyama vya kisiasa,Upande Mwingine unakosoa Muundo wa Serikali tatu kwa kigezo  cha Gharama kubwa za kuendesha Serikali tatu  Pamoja na kuhofia kuvunjika kwa Muungano.
Huku upande Mwingine Umekua ukisisitiza Serikali tatu kama Suruhisho  Pekee la Kero za Muungano.
Kwa kiasi kikubwa Wadau mbalimbali Wameipongeza Tume Ya Mbadiriko ya Katiba kwa Kuainisha vipengele Muhimu vyenye maslahai ya Taifa.
Kiu kubwa YaWatanzania ilikua ni juu ya Madaraka na Kinga ya Raisi kuona vinapunguzwa,kipengele Ambacho kimeainishwa vizuri katika Rasimu ya Katiba.
Masuala mengine yaliyopongezwa ni juu ya Mfumo Mpya wa Bunge,kuhusu Upatikanaji wa Spika kutokua Mbunge,Mawaziri kutokua Wabunge na Idadi ndogo ya Mawaziri, n.k
Mabaraza ya katiba yanaendelea kutoa Mapendekezo Kwenye Rasimu ya Katiba Mpya,Baada ya Mapendekezo ya Mabaraza ya Katiba,Bunge la Katiba litapata nafasi ya Kuijadili rasimu hiyo ya Katiba hatua itakayofuatiwa na Kura Ya Wanachi ya Kuikubali au kuikataa Katiba itakayokua imependekezwa Na Bunge la Katiba;
Kwa mujibu wa Taarifa za Mwanzo,Katiba Mpya inatarajiwa kukamilika kabla Ya Uchaguzi Mkuu Mwaka 2015.
Napenda kutoa wito kua Uchangiaji wa Maoni mbalimbali  juu ya Rasimu ya Katiba Ulenge Maslahi ya Nchi yetu kwa Maendeleo ya Taifa letu.
Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Bariki Mchakato wa Upatikanaji wa Katiba Mpya.