Makamu wa Raisi Mh,Ghalib Bilal akionyesha ishara ya uzinduzi wa Rasimu ya Katiba Mpya.Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiriko ya Katiba Jaji Msaafu Joseph Warioba na Kushoto kwake ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda.
1/8/2013
NAIPENDA NCHI YANGU
By Fabian Balele(Mwananchi Mzalendo)
Mchakato wa Upatikanaji wa katiba Mpya nchini
unaendelea huku kukiwa na Mijadala
mbalimbali inayofanyika miongoni mwa Taasisi,mashirika Binafsi,vyama vya siasa
na Wadau mbalimbali.
Kumekua na Maoni mbalimbali miongoni mwa
Wachangiaji kuhusu vipengele Mbalimbali kama vilivyopendekezwa na Tume ya
Mabadiriko ya Katiba Nchini, Chini ya Jaji Mstaafu,Joseph Warioba.
Miongoni mwa Vipengele vilivyoshika nafasi ya Juu
katika uchangiaji wa Rasimu ya Katiba Mpya ni Pamoja na Muundo wa Serikali
tatu,Umri wa Mgombea Uraisi,Maadili ya Viongozi wa Uma na Haki za Raia.
Kumekua na mvutano mkali juu ya Muundo wa
Serikali tatu hasa katika vyama vya kisiasa,Upande Mwingine unakosoa Muundo wa
Serikali tatu kwa kigezo cha Gharama kubwa
za kuendesha Serikali tatu Pamoja na
kuhofia kuvunjika kwa Muungano.
Huku upande Mwingine Umekua ukisisitiza Serikali
tatu kama Suruhisho Pekee la Kero za
Muungano.
Kwa kiasi kikubwa Wadau mbalimbali Wameipongeza
Tume Ya Mbadiriko ya Katiba kwa Kuainisha vipengele Muhimu vyenye maslahai ya
Taifa.
Kiu kubwa YaWatanzania ilikua ni juu ya Madaraka
na Kinga ya Raisi kuona vinapunguzwa,kipengele Ambacho kimeainishwa vizuri
katika Rasimu ya Katiba.
Masuala mengine yaliyopongezwa ni juu ya Mfumo
Mpya wa Bunge,kuhusu Upatikanaji wa Spika kutokua Mbunge,Mawaziri kutokua
Wabunge na Idadi ndogo ya Mawaziri, n.k
Mabaraza ya katiba yanaendelea kutoa Mapendekezo
Kwenye Rasimu ya Katiba Mpya,Baada ya Mapendekezo ya Mabaraza ya Katiba,Bunge
la Katiba litapata nafasi ya Kuijadili rasimu hiyo ya Katiba hatua
itakayofuatiwa na Kura Ya Wanachi ya Kuikubali au kuikataa Katiba itakayokua
imependekezwa Na Bunge la Katiba;
Kwa mujibu wa Taarifa za Mwanzo,Katiba Mpya
inatarajiwa kukamilika kabla Ya Uchaguzi Mkuu Mwaka 2015.
Napenda kutoa wito kua Uchangiaji wa Maoni
mbalimbali juu ya Rasimu ya Katiba
Ulenge Maslahi ya Nchi yetu kwa Maendeleo ya Taifa letu.
No comments:
Post a Comment