Kuwapo Kwa mimea inayotoa Maua yanayotoa chakula cha nyuki cha kutosha, Kwa mfano,sehemu yenye misitu, shamba la miti au mazao ya kilimo. Muda wa mimea kuchanua ujulikane kwa mfugaji nyuki ili aweze kupanga muda ambao atawezesha kundi la nyuki kujijenga na kukusanya mazao ya kutosha wakati mimea inapochanua Maua.
Maji ya kutosha ni muhimu, nyuki huyatumia kupooza kupooza joto ndani ya mzinga, kulainisha chakula na kurekebisha utamu wa asali ambayo hulishwa majana.
Mahali panapofikia ili kuwezesha usafirishaji wa vifaa na mazao ya nyuki nyakati za uvunaji.
Umbali wa kilomita tatu kutoka katika makazi ya watu,shule,hospitali na pasiwe mahali ambapo ni mapito ya Mifugo. Inapolazimu kuwa na Manzuki katika maeneo haya ,izungushiwe uzio wenye miti mirefu ili nyuki wanapokwenda nakurudi kutafuta cha kula wapiti juu ili wasishambulie watu na wanyama. Umbali uliotajwa hapa ni kwa ajili ya nyuki wanaouma tu.
Mbali na maeneo ya kilimo kinachotumia kemikali kwa mfano kilimo cha tumbaku na korosho, Manzuki yaanzishwe umbali wa kilometa saba kutoka maeneo hayo. Hii ni kuzuia nyuki wasife kwa kemikali hizo, au kuzuia mizinga isiangushwe na pia kusababisha nyuki washindwe kurudi kwenye mizinga.
Kudhibiti uharibifu kutokana na maadui wa nyuki, wizi wa mizinga na mazao ya nyuki.
Viashiria
Vifuatavyo hutumika sehemu mbalimbali kutambua muda wa kuvuna Asali..
i)Mwisho wa
Msimu wa mvua na mwanzo wa Kangazi
ii)Maua au matunda
ya mmea Fulani kupukutika
iii)Matunda ya
mmea mwitu kutokeza
iv) Mazao ya
shamabani kukomaa
v)Mng’urumo wa
nyuki wakusanyao chakula kupungua
vi)Madume ya
nyuki kuonekana yamekufa kwenye mlango ama chini ya mzinga
vii)Kundi la
Nyuki kutanda nje ya Mzinga
viii)Gundi
nyingi kuonekana katika mlango na matundu ya Mzinga
ix) Uzito wa
Mzinga kuongezeka
x)Kijiti
kuchomwa ndani ya Mzinga na kuona kama kina asali(Ukaguzi wa kienyeji)Njia hii
haimuwezeshi mfugaji kujua kama asali imeiva ama mbichi.
xi)Sauti ya mzinga
unapogongwa,inaashiria kama mzinga umejaa ama ni mtupu.
xii)Mwinamo wa
mzinga kubadilika.
Muda wa
Uvunaji asali baada ya kundi kuingia kwenye mzinga hutegemea mambo yafuatayo;
i)Kiwango cha
maua yanayopatikana kwenye eneo la shamba la nyuki.
ii)Muda ambao
maua hayo yanapatikana.
iii)Hali ya Hewa
ya eneo hilo
iv)Ukubwa wa
Kundi
No comments:
Post a Comment