Sunday, December 8, 2013

MATUKIO NA PICHA:MAHAFALI YA 29 (2013) CHUO KIKUU CHA SOKOINE MOROGORO

Tarehe 29 Novemba 2013 Kumefanyika Mahafali ya 29 Chuo kikuu cha Sokoine Morogoro.

Jumla ya Wahitimu 2548(1712-ME,836-KE) Wametunukiwa Shahada Mbalimbali,Ambapo kati yao 2017 ni Wahitimu wa Shahada  ya Kwanza(Bachelor), 313 Shahada ya Uzamili(Masters),22 Shahada ya Juu(PhD)- Udaktari wa Falsafa na Wahitimu 196 Wametunukiwa Stashahada na Cheti(Non Degree Programs-Deploma & Certificates).

Jumla ya Wahitimu 7 Wamepata Ufaulu wa Daraja La Kwanza(First Class For Undergraduate).
Wawili kutoka Kitivo Cha Kilimo(Agriculture General & Foos science and Tecnology),Wane kutoka Kitivo Cha Misitu na Hifadhi ya Mazingira(Forestry-3, & Wildilife 1 ),na Mmoja kutoka kitivo cha Sayansi(Informatics)
 
Mahafali hayo Yalihudhuliwa 
na Mkuu wa Chuo Hicho Hon. Al Noor Kassum,Makamu mkuu wa Chuo Prof Monela,Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Mh. Philemon Luhanjo Pamoja na Naibu Makamu wa Chuo Fedha na Utawala Prof Matovero,na Naibu Makamo wa Chuo Elimu Prof Gilla. Pamoja na Wakuu wa Vitivo Mbalimbali Chuoni Hapo.


Add caption

HIVI NDIVYO ILIVYOKUA KUHUSU "FRESHERS' GET TOGETHER BAASH" NA BELLE 9 @ GRONENCY HOTEL.

SUASO Kupitia Wizara ya Michezo siku ya Leo 7/12/2013 imefanikiwa kuandaa Bonanza pamoja na Burudani ya Mziki iliyomshirikisha Mwanamziki wa Kizazi kipya Belle 9 katika Hotel Maarufu Mjini Morogoro(Gronency Hotel).

Burudani hiyo ilikusudia kuwakaribisha Wananchuo wote wa Mwaka wa Kwanza Chuo Kikuu Cha Sokoine(SUA) Morogoro.
Safari ya Kuelekea Gronency Hotel ilianza mida ya sa 3 Usiku kutoka Campus zote mbili.
Makamo Rais-(SUASO) Bwn Leonard Shoo alikua ni Mgeni Rasmi katika Tamasha Hilo.
MC Makini kabisa Mwanadada wa kipekee ndo ali Host Show Nzima Siku Hiyo.
Bwn Leonard Shoo,Makamo Rais(SUASO)Akitoa neno la Kuwakaribisha Freshers siku Hiyo.
Wadau mbalimbali kutoka SUA Wakifatilia Tamasha hilo.
Msanii wa Kizazi Kipya Belle 9 Alitumbuiza katika Tamasha Hilo.
Ukafika Mda wa Kuserebuka na Kuchezesha Nyonga, Daah,Ilikuwa Nouma sana.