Wednesday, October 23, 2013

WANAFUNZI 1,107 KUNUFAIKA NA MKOPO.

                       Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Philipo Mulugo.

Serikali kupitia wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imetoa taarifa kua wanafunzi wapatao 1,107 ambao walikosa Mkopo hapo mwanzo kutokana na dosari  mbalimbali kwenye fomu zao za kuomba mkopo watanufaika na Mkopo.

Hayo yalisemwa na Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mh.Philipo Mulugo mbele ya kamati ya Kudumu ya Bunge Ya Maendeleo ya Jamii.

Wanafunzi watakaonufaika ni wanafunzi wa Masomo ya Ualimu wa sayansi(164),Ualimu-Hisabati(20),sayansi na tiba(111),Uhandisi wa Umwagiliaji(7),ualimu(617),sayansi ya kilimo(20),Sayansi(98),Uhandisi (70).

Waziri Mulugo alisema majina ya Wanufaika hao yatatangazwa na Bodi,wanafunzi wa Masomo ya Kipaumbele wamepewa nafasi hii ya kurekebisha dosari zao kupitia Bodi ya Mkopo.

Aidha alidai kua Pesa hiyo ni nje ya Pesa iliyotengwa kwa Ajili ya Mikopo ya Wanafunzi kwani baada ya Kutokea Dosari kwenye fomu zao Pesa hizo walipewa Wanafunzi wengine.

No comments:

Post a Comment