Monday, December 28, 2015
Mambo 10 Usiyoyajua Kuhusu Maisha ya "Nyuki"
1)Nyuki Malkia ni mkubwa kuliko Nyuki wengine katika kundi la Nyuki.
2)Nyuki Malkia ni jike pekee katika kundi la Nyuki mwenye uwezo wa kimaumbile wa kutaga mayai ingawaje kwenye kundi la Nyuki kuna majike wengi.
3)Nyuki Malkia ndiye Nyuki pekee mwenye uwezo wa kuishi muda mrefu zaidi,miaka mitatu hadi sita.
4)Nyuki VIBARUA ni majike ambao maumbile yao hayana uwezo wa kutaga mayai wala kujamiiana.
5)Nyuki dume hutokana na mayai ya Malkia yasiyorutubishwa na mbegu za kiume na kuwafanya nyuki hao kuwa na mzazi mmoja pekee yaani mama.
6)Nyuki dume hawana mshale wa sumu kwa ajili ya kujilinda dhidi ya maadui,badala yake wana uume.
7)Dume mmoja huweza kujaniiana na Malkia Mara moja tu ktk maisha take.
8)Baada ya tendo la kujamiiana Nyuki Dume hufa SAA chache kutokana na uume wake kukatika wakati wa kujamiiana.
9)Kwa hali hii,hata Nyuki vibarua hawajawahi kuwaona baba zao.
10)Kuna takribani aina tofauti elfu ishirini (20,000) za Nyuki wanaouma Duniani.
©Exclusive to "Balele Mwanahabari"..
Kwa maoni/Ushauri
0768937884
fabianbalele@gmail.com
SIFA ZA SHAMBA LA NYUKI (MANZUKI)
Kuwapo Kwa mimea inayotoa Maua yanayotoa chakula cha nyuki cha kutosha, Kwa mfano,sehemu yenye misitu, shamba la miti au mazao ya kilimo. Muda wa mimea kuchanua ujulikane kwa mfugaji nyuki ili aweze kupanga muda ambao atawezesha kundi la nyuki kujijenga na kukusanya mazao ya kutosha wakati mimea inapochanua Maua.
Maji ya kutosha ni muhimu, nyuki huyatumia kupooza kupooza joto ndani ya mzinga, kulainisha chakula na kurekebisha utamu wa asali ambayo hulishwa majana.
Mahali panapofikia ili kuwezesha usafirishaji wa vifaa na mazao ya nyuki nyakati za uvunaji.
Umbali wa kilomita tatu kutoka katika makazi ya watu,shule,hospitali na pasiwe mahali ambapo ni mapito ya Mifugo. Inapolazimu kuwa na Manzuki katika maeneo haya ,izungushiwe uzio wenye miti mirefu ili nyuki wanapokwenda nakurudi kutafuta cha kula wapiti juu ili wasishambulie watu na wanyama. Umbali uliotajwa hapa ni kwa ajili ya nyuki wanaouma tu.
Mbali na maeneo ya kilimo kinachotumia kemikali kwa mfano kilimo cha tumbaku na korosho, Manzuki yaanzishwe umbali wa kilometa saba kutoka maeneo hayo. Hii ni kuzuia nyuki wasife kwa kemikali hizo, au kuzuia mizinga isiangushwe na pia kusababisha nyuki washindwe kurudi kwenye mizinga.
Kudhibiti uharibifu kutokana na maadui wa nyuki, wizi wa mizinga na mazao ya nyuki.
Viashiria
Vifuatavyo hutumika sehemu mbalimbali kutambua muda wa kuvuna Asali..
i)Mwisho wa
Msimu wa mvua na mwanzo wa Kangazi
ii)Maua au matunda
ya mmea Fulani kupukutika
iii)Matunda ya
mmea mwitu kutokeza
iv) Mazao ya
shamabani kukomaa
v)Mng’urumo wa
nyuki wakusanyao chakula kupungua
vi)Madume ya
nyuki kuonekana yamekufa kwenye mlango ama chini ya mzinga
vii)Kundi la
Nyuki kutanda nje ya Mzinga
viii)Gundi
nyingi kuonekana katika mlango na matundu ya Mzinga
ix) Uzito wa
Mzinga kuongezeka
x)Kijiti
kuchomwa ndani ya Mzinga na kuona kama kina asali(Ukaguzi wa kienyeji)Njia hii
haimuwezeshi mfugaji kujua kama asali imeiva ama mbichi.
xi)Sauti ya mzinga
unapogongwa,inaashiria kama mzinga umejaa ama ni mtupu.
xii)Mwinamo wa
mzinga kubadilika.
Muda wa
Uvunaji asali baada ya kundi kuingia kwenye mzinga hutegemea mambo yafuatayo;
i)Kiwango cha
maua yanayopatikana kwenye eneo la shamba la nyuki.
ii)Muda ambao
maua hayo yanapatikana.
iii)Hali ya Hewa
ya eneo hilo
iv)Ukubwa wa
Kundi
AINA ZA NYUKI NA TABIA ZAO
Nyuki
ni jamii ya wadudu wenye jozi mbili za mabawa mepesi yenye mishipa laini.Nyuki
huishi maisha ya kijamaa.Mwili wa Nyuki umegawanyika katika sehemu kuu
tatu;kichwa ,kifua na tumbo(fumbati).Tofauti na wadudu wengine,nyuki
hutengeneza na kuhifadhi Asali kwenye masega.
Kuna
takribani aina tofauti elfu ishirini(20,000) Duniani.Nyuki hawa wanatofautiana
kwa maumbile,ukubwa na tabia,lakini wote wanashahabiana kwa tabia moja ya
kutembelea maua ili kukusanya mbochi(maji matamu yanayotengeneza asali) na
chavua(unga unaopatikana kwenye maua) kwa ajili ya chakula chao.
Kuna
jamii kuu mbili za Nyuki wanaopatikana Tanzania;Nyuki wanaouma na wasiouma.
NYUKI
WANAOUMA
Nyuki
wanaouma wanaopatikana Tanzania wamegawanyika katika makundi matatu kutegemea
mahali wanapoishi.Wapo nyuki wanaoishi;
Sehemu
za Mwambao(Pwani) wana umbo dogo na niwakali(Apis mellifera litorea),sehemu
kame na tambarare,wana umbo la wastani,wakali kiasi na hutoa asali kwa
wingi(Apis mellifera scutellata),sehemu za milimani,(zaidi ya futi 6,000 kutoka
usawa wa Bahari) wana umbo kubwa na wapole,jina la kitaalamu wanaitwa Apis
mellifera monticola.
NYUKI
WASIOUMA
Nyuki
wasiouma wanapatikana nchi za tropiki tu kama ilivyo Tanzania.
Nyuki
wasiouma wanaishi ndani ya matundu ya miti,chini ya matawi makubwa ya
miti,kwenye vichuguu vya mchwa na hata chini ya mapaa ya nyumba,nyuki hawa hu
toa asali kidogo kulinganisha na nyuki wanaouma,Nyuki wasiouma wanaweza kutoa
hadi lita 5 za asali kwa mwaka kutegemea na ukubwa wa mzinga,aina ,wingi wa
nyuki na uwepo wa chakula(maua) cha kutosha.Asali ya Nyuki wasiouma inaaminika
kuwa na uwezo mkubwa wa kutibu maradhi mablimbali kuliko asali ya Nyuki
wanaouma.
JINSIA
YA NYUKI NA MAJUKUMU YAO.
Kama
ilivyo kwa viumbe vyote,nyuki nao waa jinsia mbili,nyuki dume na Nyuki
Jike.Jinsia hizo ndiyo msingi wa mgawanyo wa majukumu ya kazi katika kundi la
Nyuki.
Kundi
la Nyuki wanaouma,lina aina tatu za Nyuki ambao ni Nyuki vibarua,malkia na
dume.
NYUKI
JIKE.
Jinsia
hii inamakundi mawili ya nyuki amabyo hutekeleza majukumu mawili tofauti.
a)Nyuki
Malkia
NYUKI MALKIA(QUEEN) |
Ni
nyuki jike ambaye hulelewa kwa kula chakula rasmi(maziwa ya Nyuki) na kupata
matunzo maalumu kwa maisha yake yote(tangu hatua ya yai hadi uzee wake
wote)Chakula hiki humwezesha kuishi kati ya miaka miwili hadi sita.
Nyuki
malkia ni mkubwa kuliko nyuki wengine katika kundi la Nyuki,tumbo lake ni refu
lenye rangi ya njano na dhahabu ghafi.
Nyuki
Malikia,hutoa kemikali(Pheremones)mwilini mwake kutoa miongozo kwa kundi la Nyuki.Mpangilioo wote na
Mgawanyo wa kazi katika kundi la nyuki hutegemea maelekezo yake.Kundi la Nyuki
lisilo na Malkia hukosa mwelekeo na huishi kwa kipindi kifupi.
b)Nyuki
Vibarua
Nyuki
vibarua ni majike ambao maumbile yao hayana uwezo wa kutaga mayai wala
kujamiiana na nyuki madume.Kwa kawaida nyuki vibarua ambao hawatagi mayai,ni
majike tasaambao hawana uwezo wa wa kutaga mayai.Aidha,hufikia kuishi hadi siku
36.Wanaweza kufikia idadi ya 60,000 au zaidi katika kundi moja.
c)Nyuki
dume
Hutokana
na mayai ya Malikia yasiyorutubishwa na mbegu za kiumena kuwafanya nyuki hao
kuwa na mzazi mmoja tu yaani mama,Nyuki dume ni wakubwa kuliko vibarua lakini
wadogo kuliko Malkia.Macho yao ni makubwa na miili yao ina rangi nyeusi,nyuki
dume hawana mshale wa sumu kwa ajili ya kujilinda dhidi ya maadui,badala yake
wana uume.
Kazi
kubwa ya Nyuki dume ni kujamiiana na malkia.Dume mmoja huweza kujamiiana na
malikia mara moja katika maisha yake.,Baada ya Tendo la kujamiiana Dume hufa saa
chache kutokan na uume wake kukatika wakati wa kujamiiana.
Kwa
hali hii hata Nyuki vibarua hawajawai kuwaona baba zao.!
Kazi
ya pili ya Nyuki madume ni kurekebisha hali ya hewa ndani ya mzinga kwa kupasha
joto kiota hasa wakati wa Usiku kwa kukumbatia juu ya kiota,sehemu ya
watoto.Wakati wa upungufu mkubwa wa chakula au kiangazi nyuki madume hutolewa
na vibarua nje ya mizinga na baadea hufa kwa njaa au baridi.
Kwa Maoni/Ushauri
0768937884
fabianbalele@gmail.com
Kwa Maoni/Ushauri
0768937884
fabianbalele@gmail.com
Subscribe to:
Posts (Atom)