Sunday, March 31, 2013

HIVI NDIVYO TAMASHA LA PASAKA(2013) LILIVYOFANA MOROGORO

Tamasha la Pasaka Mjini Morogoro lililofanyika Jamhuri Stadium limefana Baada ya Waimbaji mabalimabli wa nyimbo za Injili kuonyesha umahili wa hali ya juu walipokua wakitumbuiza kwa nyimbo zao.

Tamasha hilo lililoandaliwa na Qs Mhonda J Entertainment limewashirikisha waimbaji mabalimbali wa Morogoro huku Waimbaji kutoka Dar es Salaam wakihitimisha na kuonyesha umahili mkubwa .

Muimbaji Catherine John kutoka Morogoro akitumbuiza
mwanzo wa Tamasha hilo.
Revina Steven kutoka Morogoro naye akafatia
katika kumwimbia Bwana.
Bahati Bukuku na Stara Thomas wakienda kumtuza Muimbaji Catherine John
Walishindwa kujizuia baada ya Catherine John kuzikosha nyoyo zao na Mashabiki kwa ujumla
JGM Choir Kutoka Mororgoro nao wakafatia.


Haleluya  Choir Kutoka Morogoro wakionyesha manjonjo kwa style mbalimbali katika kumwimbia Bwana.
 Stara Thomas amabye sasa ni muimbaji wa Nyimbo za Injili akifikisha ujumbe wa Mungu kupitia Nyimbo.
Emanuel Mgaya (Masanja)a.k.a Mchungaji Mtarajiwa akimkaribisha Jukwaani Stara Thomas
Masanja kwa sasa amekua akiimba nyimbo za Injili huku akieleza nia ya kua Mchungaji hapo Baadae.
Mkurugenzi wa QS Mhonda J Entertainment(waandaaji wa Tamasha) akimuelekeza Emanuel Mgaya(Masanja) jinsi ya Kuendesha shughuli za Tamasha hilo.


Muimbaji Mkongwe wa nyimbo za Injili Bahati Bukuku akionyesha umahili wake wa kueneza Injili kupitia Nyimbo za Injili.

 Joseph Nyuki akionyesha umahili wake,
alizikosha nyoyo za mashabiki na wapenzi wa Nyimbo za Injili babada ya kulitawala jukwaa kupitia style zake za kipekee kwa Kucheza na kuruka.

Rafiki Gospel Singers kutoka jijini Dar es Salaam waionyesha manjonjo katika kumwimbia Bwana.

Martha Mwaipaja Mwenye Microphone akionyesha umahili wake katika kumwimbia Bwana.
JUKWAANI: Wapenzi wa Nyimbo za Injili waliojitokeza Mjini Morogoro katika Tamasha hilo.




Saturday, March 30, 2013

ONYESHA UZALENDO KWA VITENDO,SISITIZA MATUMIZI YA BIDHAA ZA KITANZANIA("MADE IN TANZANIA) NDIO KAULI YETU.


RASTAFARIAN- MOSSEAH ABRAHAMU Ni mdau mkubwa katika Biashara za Bidhaa mbalimbali za Kitanzania Ndani ya Jiji la Mwanza.

Rasi Mosseah aliifahamisha Blog hii kua alichagua kujihusisha na biashara ya bidhaa za asili kutoka Tanzania kwa kua yeye binafsi anapenda kuitangaza Tanzania na kuuthibitisha uzalendo kwa vitendo.

Alibainisha kua kwa kiasi kikubwa Watanzania hawapendi kununua bidhaa za nyumbani na wamekua wakinunua bidhaa za nje kwa kisingizio cha ubora hali ambayo alidai kua si kweli kua bidhaa zetu hazina ubora bali ni utamaduni mbaya tuliouzoea.

Wadau mbalimbali wamekua wakisistiza kutumia bidhaa zinazotengenezwa nyumbani ili kuimarisha uchumi.

Rasi Abrahamu aliiomba serikali kuwawezesha wadau wote wanaojihusisha na bidhaa za nyumbani kimtaji na kuwaongezea taaluma za kiujasiriamali.





KULIA:Ni baadhi ya wanunuzi  kutoka nyumbani(Tanzania).
Kwa mujibu wa Rasi Abrahamu,Wanunuzi kutoka Nyumbani ni wachache sana ukilinganisha na wanunuzi wa Kigeni.





































KUSHOTO:RASI MOSSEAH ABRAHAMU Akinionyesha baadhi ya bidhaa zinazopatikana katika duka lake la WEUSI WA KALE WAENZI @ ART GALARY



JUU KABISA: NI BIDHAA ANAZOUZA RASI ABRAHAMU



WASILIANA NA RASI MOSSEAH ABRAHAMU KUPITIA    +255   ( 0)767175778
                                                                                                                    ( 0)785978580
                                                                                                                    ( 0)716902246

BARABARA YA KAPRI POINT NDANI YA JIJI LA MWANZA.

Friday, March 29, 2013

TAMASHA KUBWA LA PASAKA MOROGORO,WAIMBAJI MAARUFU WA NYIMBO ZA INJILI KUWASHA MOTO.

Tamasha kubwa la injili linatarajiwa kufanyika siku ya J'PIL Siku Ya Pasaka, Jamhuri Stadium.
Waimbaji Wakubwa Wa Injili Wanatarajiwa kutumbuiza Siku Hiyo.
Miongoni Mwa Waimbaji hao ni:
      Masanja,Bahati Bukuku,
      Martha Mwaipaja
      Joseph Nyuki
      Stara Thomasi 
      Rafiki Gospel Singers Pia wanatarajiwa kutumbuiza siku hiyo.
Kwa Mujibu wa Qs Mhonda  J Entertainment Kiingilio kwa wakubwa inatarajiwa kuwa sh 5000/= Na Sh. 3000 Kwa Watoto.


Wednesday, March 27, 2013

WAFAHAMU WABUNGE VIJANA WALIOHITIMU JKT SIKU YA JANA.

Wabunge Vijana kadhaa siku ya jana tarehe 26 March 2013 wamehitimu mafunzo ya JKT.
Wabunge hao vijana wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania Waliungana na Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu kidato cha sita mwaka 2013 ikiwa ni Programu maalumu kwa ajili ya kujenga uzalendo  kwa vijana katika taifa letu.


Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma Kaskazini mbele kushoto na Idd Azan (KATIKATI)wakionyesha UKAKAMAVU katika mafunzo ya JKT kambi 835 KJ.




KULIA: Mh. Zitto kabwe akikabidhiwa cheti cha kuhitimu Mgambo JKT Na Mkuu wa Wilaya ya Handeni.









KUSHOTO:Mbunge wa Biharamulo Mh.Athanas Mbassa akila kiapo katika kambi ya Mgambo JKT Tanga.












KULIA: Mh. Abdalah Hjji Ally Mbunge wa Kiwani Pemba kambi ya Mgambo JKT TANGA










KUSHOTO:  Mh. Raya Ibrahimu Khamisi.(mbunge wa viti maalimu CHADEMA)












KULIA: Mh. Halima Mdee(wa kwanza kulia) na Waheshimiwa wenzake akila kiapo.





Amiri Jeshi Mkuu Na Raisi wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania Akimkabidhi Cheti cha Kuhitimu mafunzo ya Mgambo JKT Mh. Esther Bulaya kambi ya Ruvu JKT.











KULIA: Mh. Livingstone Lusinde Mb. wa Mtera.(watatu kutoka mbele mstari wa kwanza)







Picha kwa Msaada wa Mtandao na Jamii Forum.

Friday, March 15, 2013

SIKU YA MATEMBEZI YA MSHIKAMANO KUWAKUMBUKA NA KUWAENZI AKINA MAMA WALIOFARIKI KWA MATATIZO YA UZAZI

Jana tarehe 15 March 2013 kumefanyika Matembezi maalumu ya kuwakumbuka akina mama waliofariki kwa matatizo ya uzazi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Utepe Mweupe.

Maadhimisho ya siku ya Utepe Mweupe yalizinduliwa rasmi Mwaka 2006 Na Raisi wa Awamu ya pili ndg. ALLY HASSAN MWINYI Kwa lengo la kuwahamasisha viongozi kupanga mikakati mbalimbali ili kupunguza vifo vya akina Mama Wajawazito.

Kitaifa Matembezi Hayo yamefanyika Mkoani Mwanza kuanzia Hospitali ya mkoa -Sekoutoure hadi viwanja vya Nyamagana hapa jijini Mwanza.

Mgeni rasmi alikua Naibu Waziri, Wizara ya Afya na ustawi wa jamii ambaye pia ni mbunge wa Rufiji Mh, Dk. Seif Rashidi.
Kauli mbiu  kwa mwaka huu katika Maadhimisho hayo ni "TUTOKOMEZE VIFO VYA MAMA NA MTOTO MCHANGA"

Naibu waziri, Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Dk.Seif Rashid Akikagua Banda la Maonyesho kutoka Shirika la World Vision katika viwanja vya Nyamagana.
World Vision ni mdau Mkubwa katika kupunguza vifo vya Mama na Mtoto kupitia huduma mbalimbali za jamii wanazotoa.

Stara Thomas katikati Mwanamziki Mashuhuri wa kike Tanzania ambaye ni Balozzi wa Utepe Mweupe Tanzania akiimba nyimbo za kuhamasisha jamii kupunguza vifo vya mama na mtoto katika maadhimisho hayo.


Kushoto ni mratibu wa Maadhimisho ya Utepe mweupe na uzazi salama kitaifa Bi.Rose Mlai akieleza maana ya utepe mweupe kua ni Alama ya Matumaini,vilivile ni kuhuzunika kawa vifo vya akina mama wanaopoteza maisha kwa matatizo ya Uzazi.

Vilevile aliiomba serikali kuboresha huduma za uzazi salama Vijijini,mashuleni na vyuoni.

Aliwaasa akina baba kutoa ushirikiano wa kutosha pindi Mama anapopata ujauzito hadi kujifungua.

Alitahadharisha Akina mama wanaotumia njia za kienyeji kwa kujifungua kua si salama.
Aliwaomba Wabunge Kutumia fursa waliyonayo kwa kupitisha Bajeti ya kutosha katika huduma za akina mama wajawazito.



KULIA: Mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza akibainisha kua Vifo vya Akina mama vimeshuka kutoka vifo 200 @ Akina Mama 100,000 waliokatika hali ya kujifungua kwa mwaka 2008 kufikia vifo 160 Mwaka 2012.
Bado kuna changamoto kubwa kwani idadi hiyo ni kubwa.

Vilevile alibainisha kua Hali ya Uzazi wa Mpango kwa mkoa wa Mwanza iko chini sana ambayo ni asilimia 14.(14%) Pekee.

Kwa takwimu hizo inaonesha kua kila siku Wanawake 20 Walio katika hali ya Ujauzito wanapoteza Maisha.
Aliiomba serikali kuongeza idadi ya watoa huduma za afya,mazingira bora ya Watumishi wa afya hasa Wakunga na kuongeza vifaa tiba.

Mgeni Rasmi,Naibu waziri,wizara ya afya na Ustawi wa Jamii Dk. Seif Rashid alibainisha kua Serikali inapiga hatua kupunguza idadi ya vifo vya Mama mzazi na Watoto.

Alibainisha kua Tanzania ni nchi ya 6 Afrika katika kupunguza vifo vya Mama na Mtoto.
Aliiomba jamii kuongeza bidii kwa kushirikiana na serikali ili kutokomeza kabisa vifo vya Mama na Mtoto.
Aliwaasa akina Mama kudai haki za Hiuduma za uzazi kwani ni haki yao.
Pia kila Mwanajamii ashiriki kikamilifu katika kuzuia vifo vya Mama na Mtoto.
Akina Baba Washiriki kikamilifu  katika kutoa Msaada wakati wa Mama awapo mjamzito.

Katika maadhimisho hayo pia kulikua na Brudani kama inavyoonekana hapa chini.


Thursday, March 14, 2013

MAADHIMISHO YA SIKU YA PAI(22/7) SULE ZA SEKONDARI JIJINI MWANZA
















Leo tarehe 14.3.2013 Ni siku ya kumbukumbu ya Pai Duniani.
Ni siku maalumu ambapo Mtu aliyegundua Pai  (22/7) anakumbukwa.

Kwa Dar es Salaam Maadhimisho hayo yanafanyika katika viwanja vya mnazi mmoja.
Kwa hapa Mwanza ikiwa ni mara ya kwanza kwa maadhimisho hayo kufanyika kwa shule za sekondari jijini Mwanza,Maadhimisho  yamefanyika katika Shule ya sekondari ya Mwanza.

Lengo kubwa la maadhimisho hayo ni kuwapa hamasa wanafunzi kote nchini juu ya Somo la Hisabati.

Mengi yameongelewa ikiwa ni pamoja na Kuendelea kushuka kwa ufaulu wa somo la Hisabati mwaka hadi mwaka.


Kushoto ni Mlezi wa Chama cha Hisabati Tanzania(CHAHITA)Kanda ya Mwanza,
Ambae pia ni mkuu wa Shule ya Sekondari ya Pamba akibainisha baadhi ya Changamoto za kuendelea kushuka kwa ufaulu wa somo la hisabati.
Takwimu zinaonesha kua,
Mwaka 2008 kwa kidato cha nne ufaulu wa Somo la Hisabati kitaifa kwa madaraja ya A,B,C na D ulikua ni 9.18 %
Mwaka 2009 kwa madaraja hayo ufaulu uliendelea kushuka na kufikia 7.99 %
Mwaka 2010 ikawa 6.6 %
Mwaka 2011 ikawa 5.83 %

Vile vile kwa mwaka 2012 Takwimu zinaonesha kua kwa kanda ya Mwanza kupitia shule 13 ufaulu wa Hisabati kidato cha nne ulikua kama ifuatavyo.


Wanafunzi waliopata Daraja A walikua 8
Waliopata Daraja B walikua 39 Sawa na 1.76 % ya wanafunzi wote.
Waliopata Daraja C walikua ni wanafunzi 103 Sawa na 4.6 %
Walopata daraja D walikua ni wanafunzi 106 sawa na  4.79 % na 
Waliopata daraja F walikua ni wamnafunzi 1953 sawa na 88.41 %

                                    CHANGAMOTO ZILIZOBAINISHWA
1) Idadi kubwa ya wanafunzi kwa  darasa moja
2) Ukosefu wa semina na Warsha za Walimu kufuatilia Mitaala ambayo hubadirika mara kwa Mara.
3)Kuruhusu Elimu kua Huria Kupelekea kuwepo na watunzi wengi wa vitabu mbalimbali visivyogizi vigezo.
4)Elimu kutolewa na watu wasiokua na WELEDI(Professional) Mfano, wanafunzi kidato cha sita kua Walimu.
5)Lugha ya Mawasiliano.


Kulia ni Mwl. Dotto Lubango ambaye ni Mwenyekiti wa Wakuu wa shule za Sekondari Mkoa wa Mwanza (TAHOSSA) Akimwakilisha mgeni rasimi Afisa ELimu Mkoa.

Mwl. Lubango alishauli yafuatayo,

1)Somo la Hisabati lipewe Kipaumbele kwa kufanya mazoezi ya kutosha
2)Wanafunzi wampende Mwl anayefundisha somo husika
3)Kuanzisha kwa Mathematics Clubs Mashuleni
4)Kuwepo na Zawadi maalumu kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katika somo la Hisabati siku za Maadhimisho ya Pai Duniani
5)Walimu wawahamasishe wanafunzi kulipenda somo la Hisabati.

Mwisho kabisa Mwakilishi huyo wa Mgeni rami alikishukuru Chama cha Hisabati Tanzania kanda ya Mwanza (CHAHITA) NA MAT(Mathematics Teachers) Kwa kuandaa maadhimisho hayo ya Siku ya Pai ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika Mkoani Mwanza.

Walimu nao walipopata nafasi ya kuchangia waliwasisitiza wanafunzi kutokua watoro darasani,kuondoa mtazamo Hasi kua somo la Hisabati ni Gumu. na kufanya mazoezi ya kutosha ili kuimarisha ufaulu wa Somo la Hisabati.

Wanafunzi waliowaomba walimu kuwa na uvumilivu kwa wanafunzi na kupunguza ukali darasi kwani Somo la Hisabati linahitaji uvumilivu wa kutosha.
Vile vile waliomba walimu kufundisha kwa vitendo pale inapostahili ili kurahisisha somo la Hisabati.
Mkuu wa Sule ya Sekondari ya Mwanza akielezea Maana ya Pai(22/7)Madhumuni ya maadhimisho hayo na Historia ya Pai.

   UHUSIANO WA PAI(22/7) NA TAREHE YA MAADHIMISHO.
Tarehe ya maadhimisho ni 14 -3 , MDA WA KUMBUKUMBU SAA (1 P.M) DAKIKA YA 59 SEKUNDE YA 26.
Thamani ya Pai (22/7)  = 3.1415926
Hivyo ukichukua namaba 14 baada ya 3 kutoka thamani ya Pai(3.1415926) 
Utagundua kua tarehe ya maadhimisho yaani taraehe 14 mwezi wa 3 sa (1 P.M) dakika ya 59 sekunde ya 26 ambao ndio muda muafaka wa Tukio la kumbukumbu ya Pai... Namba zote hizo zinatoka kwenye hiyo thamani ya Pai(3.1415926)
Mwanafunzi wa Shule ya sekondari ya Nsumba akitumbuiza katika maadhimisho hayo.

WAFUNZI KUTOKA SHULE YA SEKONDARI YA SEMINARY YA ST JOSEPH WAKIONYESHA KWA VITENDO KUHUSU UMBO LA DUARA.



    WAGENI WAALIKWA  AMBAPO PIA NI WADAU WA SOMO LA HISABATI KATIKA        MAADHIMISHO HAYO YA SIKU YA PAI.
WAFUNZI KUTOKA SHULE MBALIMBALI JIJINI MWANZA WAKIFUATILIA PROGRAM U MBALIMBALI WAKATI WA MAADHIMISHO HAYO.