Leo ni siku ya wanawake Duniani.Tanzania imeungana na nchi nyingine kuadhimisha siku hii huku jambo kubwa na lamuhimu ni kuonyesha kua tunawathamini na kuwapa nafasi sawa katika jamii yetu Kiuchumi,kisiasa na mengineyo.
Nimepata mda wa kuhudhuria moja ya maadhimisho hayo.
Nilitegemea kuona uhusishwaji wa akina Mama kwa hali ya juu ikiwa ni ishara kua Wanawake wanapata fursa sawa katika nyanja mbalimbali.
Chakushangaza ni kua karibu kila nyanja mahali pale paliongozwa na akina Baba,yaani kuanzaia usalama,washehereshaji,waandishi wa habari,ma MC,PRESENTERS,na Wengineo
.
Je,Kwahali hii tunapiga hatua kuwapa fursa sawa akina Mama?
Binafsi ningependa kuona akina mama wakiwa mstari wa mbele zaidi mahali pale kuliko ilivyuokua,nafikiri kua bado kuna changamoto kubwa ya kuwawezessha akina mama.
No comments:
Post a Comment