Jana tarehe 15 March 2013 kumefanyika Matembezi maalumu ya kuwakumbuka akina mama waliofariki kwa matatizo ya uzazi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Utepe Mweupe.
Maadhimisho ya siku ya Utepe Mweupe yalizinduliwa rasmi Mwaka 2006 Na Raisi wa Awamu ya pili ndg. ALLY HASSAN MWINYI Kwa lengo la kuwahamasisha viongozi kupanga mikakati mbalimbali ili kupunguza vifo vya akina Mama Wajawazito.
Kitaifa Matembezi Hayo yamefanyika Mkoani Mwanza kuanzia Hospitali ya mkoa -Sekoutoure hadi viwanja vya Nyamagana hapa jijini Mwanza.
Mgeni rasmi alikua Naibu Waziri, Wizara ya Afya na ustawi wa jamii ambaye pia ni mbunge wa Rufiji Mh, Dk. Seif Rashidi.
Kauli mbiu kwa mwaka huu katika Maadhimisho hayo ni "TUTOKOMEZE VIFO VYA MAMA NA MTOTO MCHANGA"
Naibu waziri, Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Dk.Seif Rashid Akikagua Banda la Maonyesho kutoka Shirika la World Vision katika viwanja vya Nyamagana.
World Vision ni mdau Mkubwa katika kupunguza vifo vya Mama na Mtoto kupitia huduma mbalimbali za jamii wanazotoa.
Stara Thomas katikati Mwanamziki Mashuhuri wa kike Tanzania ambaye ni Balozzi wa Utepe Mweupe Tanzania akiimba nyimbo za kuhamasisha jamii kupunguza vifo vya mama na mtoto katika maadhimisho hayo.
Kushoto ni mratibu wa Maadhimisho ya Utepe mweupe na uzazi salama kitaifa Bi.Rose Mlai akieleza maana ya utepe mweupe kua ni Alama ya Matumaini,vilivile ni kuhuzunika kawa vifo vya akina mama wanaopoteza maisha kwa matatizo ya Uzazi.
Vilevile aliiomba serikali kuboresha huduma za uzazi salama Vijijini,mashuleni na vyuoni.
Aliwaasa akina baba kutoa ushirikiano wa kutosha pindi Mama anapopata ujauzito hadi kujifungua.
Alitahadharisha Akina mama wanaotumia njia za kienyeji kwa kujifungua kua si salama.
Aliwaomba Wabunge Kutumia fursa waliyonayo kwa kupitisha Bajeti ya kutosha katika huduma za akina mama wajawazito.
KULIA: Mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza akibainisha kua Vifo vya Akina mama vimeshuka kutoka vifo 200 @ Akina Mama 100,000 waliokatika hali ya kujifungua kwa mwaka 2008 kufikia vifo 160 Mwaka 2012.
Bado kuna changamoto kubwa kwani idadi hiyo ni kubwa.
Vilevile alibainisha kua Hali ya Uzazi wa Mpango kwa mkoa wa Mwanza iko chini sana ambayo ni asilimia 14.(14%) Pekee.
Kwa takwimu hizo inaonesha kua kila siku Wanawake 20 Walio katika hali ya Ujauzito wanapoteza Maisha.
Aliiomba serikali kuongeza idadi ya watoa huduma za afya,mazingira bora ya Watumishi wa afya hasa Wakunga na kuongeza vifaa tiba.
Mgeni Rasmi,Naibu waziri,wizara ya afya na Ustawi wa Jamii Dk. Seif Rashid alibainisha kua Serikali inapiga hatua kupunguza idadi ya vifo vya Mama mzazi na Watoto.
Alibainisha kua Tanzania ni nchi ya 6 Afrika katika kupunguza vifo vya Mama na Mtoto.
Aliiomba jamii kuongeza bidii kwa kushirikiana na serikali ili kutokomeza kabisa vifo vya Mama na Mtoto.
Aliwaasa akina Mama kudai haki za Hiuduma za uzazi kwani ni haki yao.
Pia kila Mwanajamii ashiriki kikamilifu katika kuzuia vifo vya Mama na Mtoto.
Akina Baba Washiriki kikamilifu katika kutoa Msaada wakati wa Mama awapo mjamzito.
Katika maadhimisho hayo pia kulikua na Brudani kama inavyoonekana hapa chini.
No comments:
Post a Comment