Leo tarehe 14.3.2013 Ni siku ya kumbukumbu ya Pai Duniani.
Ni siku maalumu ambapo Mtu aliyegundua Pai (22/7) anakumbukwa.
Kwa Dar es Salaam Maadhimisho hayo yanafanyika katika viwanja vya mnazi mmoja.
Kwa hapa Mwanza ikiwa ni mara ya kwanza kwa maadhimisho hayo kufanyika kwa shule za sekondari jijini Mwanza,Maadhimisho yamefanyika katika Shule ya sekondari ya Mwanza.
Lengo kubwa la maadhimisho hayo ni kuwapa hamasa wanafunzi kote nchini juu ya Somo la Hisabati.
Mengi yameongelewa ikiwa ni pamoja na Kuendelea kushuka kwa ufaulu wa somo la Hisabati mwaka hadi mwaka.
Kushoto ni Mlezi wa Chama cha Hisabati Tanzania(CHAHITA)Kanda ya Mwanza,
Ambae pia ni mkuu wa Shule ya Sekondari ya Pamba akibainisha baadhi ya Changamoto za kuendelea kushuka kwa ufaulu wa somo la hisabati.
Takwimu zinaonesha kua,
Mwaka 2008 kwa kidato cha nne ufaulu wa Somo la Hisabati kitaifa kwa madaraja ya A,B,C na D ulikua ni 9.18 %
Mwaka 2009 kwa madaraja hayo ufaulu uliendelea kushuka na kufikia 7.99 %
Mwaka 2010 ikawa 6.6 %
Mwaka 2011 ikawa 5.83 %
Vile vile kwa mwaka 2012 Takwimu zinaonesha kua kwa kanda ya Mwanza kupitia shule 13 ufaulu wa Hisabati kidato cha nne ulikua kama ifuatavyo.
Wanafunzi waliopata Daraja A walikua 8
Waliopata Daraja B walikua 39 Sawa na 1.76 % ya wanafunzi wote.
Waliopata Daraja C walikua ni wanafunzi 103 Sawa na 4.6 %
Walopata daraja D walikua ni wanafunzi 106 sawa na 4.79 % na
Waliopata daraja F walikua ni wamnafunzi 1953 sawa na 88.41 %
CHANGAMOTO ZILIZOBAINISHWA
1) Idadi kubwa ya wanafunzi kwa darasa moja
2) Ukosefu wa semina na Warsha za Walimu kufuatilia Mitaala ambayo hubadirika mara kwa Mara.
3)Kuruhusu Elimu kua Huria Kupelekea kuwepo na watunzi wengi wa vitabu mbalimbali visivyogizi vigezo.
4)Elimu kutolewa na watu wasiokua na WELEDI(Professional) Mfano, wanafunzi kidato cha sita kua Walimu.
5)Lugha ya Mawasiliano.
Kulia ni Mwl. Dotto Lubango ambaye ni Mwenyekiti wa Wakuu wa shule za Sekondari Mkoa wa Mwanza (TAHOSSA) Akimwakilisha mgeni rasimi Afisa ELimu Mkoa.
Mwl. Lubango alishauli yafuatayo,
1)Somo la Hisabati lipewe Kipaumbele kwa kufanya mazoezi ya kutosha
2)Wanafunzi wampende Mwl anayefundisha somo husika
3)Kuanzisha kwa Mathematics Clubs Mashuleni
4)Kuwepo na Zawadi maalumu kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katika somo la Hisabati siku za Maadhimisho ya Pai Duniani
5)Walimu wawahamasishe wanafunzi kulipenda somo la Hisabati.
Mwisho kabisa Mwakilishi huyo wa Mgeni rami alikishukuru Chama cha Hisabati Tanzania kanda ya Mwanza (CHAHITA) NA MAT(Mathematics Teachers) Kwa kuandaa maadhimisho hayo ya Siku ya Pai ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika Mkoani Mwanza.
Walimu nao walipopata nafasi ya kuchangia waliwasisitiza wanafunzi kutokua watoro darasani,kuondoa mtazamo Hasi kua somo la Hisabati ni Gumu. na kufanya mazoezi ya kutosha ili kuimarisha ufaulu wa Somo la Hisabati.
Wanafunzi waliowaomba walimu kuwa na uvumilivu kwa wanafunzi na kupunguza ukali darasi kwani Somo la Hisabati linahitaji uvumilivu wa kutosha.
Vile vile waliomba walimu kufundisha kwa vitendo pale inapostahili ili kurahisisha somo la Hisabati.
Mkuu wa Sule ya Sekondari ya Mwanza akielezea Maana ya Pai(22/7)Madhumuni ya maadhimisho hayo na Historia ya Pai.
UHUSIANO WA PAI(22/7) NA TAREHE YA MAADHIMISHO.
Tarehe ya maadhimisho ni 14 -3 , MDA WA KUMBUKUMBU SAA (1 P.M) DAKIKA YA 59 SEKUNDE YA 26.
Thamani ya Pai (22/7) = 3.1415926
Hivyo ukichukua namaba 14 baada ya 3 kutoka thamani ya Pai(3.1415926)
Utagundua kua tarehe ya maadhimisho yaani taraehe 14 mwezi wa 3 sa (1 P.M) dakika ya 59 sekunde ya 26 ambao ndio muda muafaka wa Tukio la kumbukumbu ya Pai... Namba zote hizo zinatoka kwenye hiyo thamani ya Pai(3.1415926)
Mwanafunzi wa Shule ya sekondari ya Nsumba akitumbuiza katika maadhimisho hayo. |
WAFUNZI KUTOKA SHULE YA SEKONDARI YA SEMINARY YA ST JOSEPH WAKIONYESHA KWA VITENDO KUHUSU UMBO LA DUARA. |
WAFUNZI KUTOKA SHULE MBALIMBALI JIJINI MWANZA WAKIFUATILIA PROGRAM U MBALIMBALI WAKATI WA MAADHIMISHO HAYO. |
No comments:
Post a Comment