Monday, December 31, 2012

MATUKIO MUHIMU 2012

Mwaka 2012 umekua mwaka  wa kihistoria kwa namna yake kutokana na matukio mbalimbali ya kisiasa,kijamii na kiuchumi kwa hapa Tanzania  na Duniani kwa ujumla.
Kwa hapa Tanzania matukio yafuatayo yalionekana kupewa nafasi ya kipekee.

1)KIFO CHA MSAANI NGULI WA FILAMU-STEVEN CHARLES KANUMBA.
Si tu kwa watu wakubwa bali hata kwa watoto wadogo,tukio la kifo cha msanii nguli wa Tasnia ya Filamu nchini na Afrika ya Mshariki hadi Afrika ya Kati kilionekana kuwahuzunisha walio wengi.
Steven Kanumba aliitangaza nchi ya Tanzania nchi za nje hasa Afrika Mshariki,Afrika ya kati na Afrika Mgharibi kupitia Tasnia ya Filamu,
Miongoni mwa filamu alizowahi kuigiza ni pamoja na THIS IS IT,UNCLE JJ,THE BIG DADDY,DEVEL KINGDOM,MOSES,BECAUSE OF YOU,YOUNGER MILLIONAIRE,THE SHOCK,DECEPTION,KIJIJI CHA TAMBUA HAKI
Steven Kanumba alizaliwa 8/1/1984 na kufariki   usiku wa Tarehe 6/4/2012








  Bi.Flora, Mama mzazi wa Kanumba.












2)KUZAMA KWA MELI YA MV.SKAGIT

Ni tukio lililoacha majonzi makubwa kwa Watanzania wa Bara na Zanzibar kwa Ujumla
Ilikua ni tarehe 18/7/2012 Meli ijulikanayo kwa jina la Mv.Skagit ya kampuni ya SEAGULL ilpozama eneo la Chumbe ikiwa na Abiria 250.
Abiria waapatao 150 waliokolewa ktk ajali hiyo.
Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo wakisubiri kuokolewa wakiwa kwenye mgongo wa meli hiyo.

    Askari wakiwa wamebeba maiti ya mmoja wa watu waliokufa ktk ajali hiyo


   HEKA HEKA ZA UBUNGE WA LEMA
Mwaka 2012 pia katika duru za kisiasa nchini Tanzania utakumbukwa kwa hekaheka za za kuvuliwa ubunge wa Godbless Lema Mbunge wa Arusha Mjini.
Jaji Mfawidhi Gabriel Rwakibarika wa Mahakama ya kanda ya Sumbawanga alimvua ubunge Lema April 5 2012.

Kesi ya Kupinga matokeo ya ushindi wa Ubunge wa Arusha mjini dhidi ya mgombea wa CCM Dr. Batilda Burian ilifunguliwa na makada wa CCM Hapiness Kivuyo,Agnes Molel na Musa Mkenga. kwa kupinga kua Lema alitumia lugha ya matusi dhidi ya Dk. Buriani kipindi cha Kampeni.

Hata hivyo Mahakama ya rufaa ilimrejesha Lema kua Mbunge halali wa Arusha Mjini baada ya Kushinda rufaa ya kesi hiyo tarehe  21 Dec 2012. 
Godbless Lema na wafuasi wa CHADEMA mara baada ya hukumu ya kupinga Ubunge wake kutolewa kua si Mbunge Halali wa Arusha mjini ktk mahakama kuu kanda ya Arusha.
 Godbless Lema na wafuasi wa CHADEMA baada ya ushindi wa rufaa yake katika makama ya rufaa jijini Dar es Salaam

KUTEKWA NYARA KWA DK. ULIMBOKA
Mwaka 2012 pia utakumbukwa kwa tukio la  mgomo wa madaktari hali iliyopelekea kupoteza maisha kwa baadhi ya wagonjwa.

Tukio kubwa ktk hekeheka za mgomo wa madaktari pia ni kutekwa nyara kwa mwenyekiti wa jumuiya ya madaktari Dk. Steven Ulimboka.

Dk. Steven Ulimboka ndiye aliyekua kiongozi wa madaktari aliyekua akiratibu suala zima la kuidai serikali itekeleze malalamiko ya madaktari ikiwemo mazingira mazuri ya kufanyia kazi,kuwepo kwa vifaa vya matibabu,posho mbalimbali kama posho ya usafiri,kufanya kazi ktk mazingira magumu.

Mdaktari pia waliitaka serikali kuwapatia Green Card za bima ya afya,kuwaondoa watendaji wakuu ktk wizara ya afya akiwemo waziri wa afya,katibu mkuu wa wizara hiyo na Mganga mkuu wa serikali.

Serikali ilitimiza baadhi ya mahitaji hayo ikiwepo kuwapatia Green card za bima ya afya,kuawaondoa waziri,katibu mkuu na Mganga mkuu wa Serikali  na mambo mengine.

Katika hali isiyo ya kawaida  Dk. Ulimboka alitekwa na watu wasiojulikana kisha kuteswa kwa kung'olewa kucha,meno na kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake kisha kutupwa katika msitu wa Magwepande ulio nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.  
Dk. Steven Ulimboka akiwa amefikishwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuokotwa na msamaria mwema ktk msitu wa Magwepande.

      Dk. Ulimboka akiendelea kupata matibabu ktk hospitali ya Taifa ya Muhimbili.hata ivyo Dk. Ulimboka alihamishiwa Afrika ya kusini kwa matibabu zaidi baada ya hali yake kubadirika.
Dk. Ulimboka katika moja ya vikao akijaribu kuonyesha msisitizo kua Serikali inapaswa kuzingatia malalamiko ya madaktari nchini.


KIFO CHA MWANDISHI WA HABARI-CHANEL TEN-DAUD MWANGOSI
Hili pia ni tukio kubwa lililoacha majonzi na simanzi kubwa miongoni mwa Watanzania.
Daudi Mwangosi aliyekuwa mwakilishi wa kituo cha utangazaji chanel ten alifariki alipokua akitekeleza majukumu yake ya kikiazi ya uandishi huko Mkoani Iringa - kijiji cha Nyororo ambapo inadaiwa kua CHADEMA kilikua kikifanya shughuli zake zakisiasa katika harakati zao za M4C.

Kufuatia kifo hicho tume mbalimbali ziliundwa kuchunguza mazingira tatanishi ya kifo chake kutokana na uvumi kua alilipuliwa na bomu la machozi,huku wengine wakidai kua alipigwa na kitu kizito kichwani.

Tume zilizoundwa ni pamoja na ile ya Mh. Nchimbi waziri wa mambo ya ndani ya Nchi pamoja na ile iliyoundwa na chama cha waandishi wa habari.

                                                      Daud Mwangosi Enzi za uhai wake

.
                  KIFO CHA MCHEZAJI WA MPIRA-PATRICK MAFISANGO
Mwaka 2012 utakumbukwa pia kwa tukio la kusikitisha la ajali  Iiyosababisha kifo cha mchezaji wa Timu ya SIMBA Patrick Mafisango.


 
Patrick Mafisango enzi za uhai wake akiwajibika ipasavyo uwanjani katika moja ya mechi za timu ya Simba.













Gari aliyokua nayo Mafisango ikiwa imeharibika vibaya baada ya ajali hiyo kutokea.






wacezaji wa SIMBA pamoja na waombolezaji wengine wakiuaga mwili wa Mafisango.









KUANZISHWA KWA TUME YA KUKUSANYA MAONI YA KUAANDAA RASIMU YA KATIBA MPYA TANZANIA.
Kuanzishwa kwa tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya Hapa Tanzania ni moja ya tukio muhimu la kukumbukwa hapa Tanzania.
Tume hii ilianzishwa rasimi na Mh. KIKWETE Raisi wa Tanzania kwa mujibu wa Katiba ya sasa.
Tume ilipewa miezi 18 kukamilisha zoezi hilo.
Kuna mategemeo makubwa ya kutumia Katiba Mpya Katika Uchaguzi ujao wa mwaka 2015.





Kushoto:Mwenyekiti wa Tume ya mabadiriko ya katiba Jaji mstaafu (Jaji Warioba) akiwa na viongozi na wanachama wa CUF walipofika ktk ofisi za Tume Hiyo Kuwasilisha Maoni ya Chama hicho.





KIFO CHA SHARO MILLIONAIRE.
2012 Utakumbukwa kwa majonzi baada ya kumpoteza Msanii wa maigizo Sharo Miliionaire Aliyefariki baada ya kupata ajali akielekea nyumbani kwao Mkoani Tanga.
                                                   Sharo Millionaire enzi za Uhai wake.



                                      UVUMI WA MIKE-TYSON KUBADILI JINSIA
Mwishoni mwa mwezi November mwaka jana 2012,Kulitokea uvumi mkubwa katika vyombo mbalimbali kua Mike Tyson Bondia wa Zamani wa Uzito wa Juu DUNIANI alibadili jinsia.
Hata ivyo uvumi huo ulikanushwa na Mike Tyson Mwenyewe kama ilivyoripotiwa na shirika la Utangazaji la BBC.

Sunday, December 23, 2012

NJIA YA KUJIPATIA UTAJIRI WA HALALI KWA VIJANA YAGUNDULIKA

Imekua ni jambo la kawaida kwa jamii ya kitanzania hasa vijana kudhani kua ni kazi za ofsini pekee zinazoweza kumkwamua kijana kutoka katika wimbi la umasikini.Vijana wengi wamekua wakikwepa kazi za nje kama vile kilimo,uvuvi,ufagaji na nyinginezo.

Wakikiongea katika kipindi maalumu cha VIJANA ktk mada ya Jinsi ufugaji wa nyuki unavyoweza kumkomboa kijana wa kitanzania kinachorushwa kila J'mosi SUA-TV vijana Kutoka Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine(SUA)-Morogoro wanaosoma shahada ya kwanza ya Misitu walithibitisha kua ufugaji wa nyuki ni njia ya haraka zaidi ya kujipatia utajiri wa HALALI.

Wkiongea katika kipindi hicho kilichoandaliwa na Tanzania Forestry Students' Association(TFSA),Wanafunzi hao  walithibitisha kua Mzinga mmoja kwa wastani unauwezo wa kuzalisha asalli lita 10,kwa bei ya lita 1 sawa na sh.10,000 iwapo utakua na mizinga 20 basi utapata kiasi cha Tsh.Milioni 2,kiasi ambacho kinaweza kumkwamua kijana kutoka ktk wimbi la umasikini.

Ufugaji wa nyuki ni shughuli rahisi isiyohitaji mtaji mkubwa kama zilivyo shughuli nyingine.

Asali hutumika kama chakula,dawa za binadamu, losheni,kuokea mikate,kukoleza tumbaku na matumizi mengineyo.
Mbali na asali nyuki pia wanazalisha inta amabayo inatumika kutengeneza bidhaa mbalimbali kama vile dawa za kulainisha ngozi,mishumaa,karatasi za kaboni na creams mbalimbali za urembo.

Tanzania ni mojawapo ya nchi Tano za Afrika zilizoruhusiwa kuuza asali yake katika soko la nje hasa la umoja wa nchi za Ulaya.

Nchi inayoongoza Afrika kwa  uzalishaji wa asali ni Ethiopia.

Nchi nyingine zilizoruhusiwa kuuza asali ktk soko hilo ni Ehiopia,Uganda,Zambia na Madagascar.

Inakadiriwa kua iwapo Ufugaji wa nyuki utapewa kipaumbele,Tanzania ina uwezo wa kuzalisha Tani 138,000 za asali kwa mwaka zenye thamani ya Bilioni 133.3.Pia inaweza kuzalisha tani 9200 za inta zenye thamani sawa na 35.5 bilion kwa mwaka.

Kwa sasa Tanzania iazalisha tani 4860 pekee za asali zenye thamani ya Sh.4.9 Bilioni na inta tani 324 sawa na 648 Milioni kwa mwaka
.
Wanunuzi wakubwa wa asali ya hapa nchini  ni Kenya,Ujerumani,Uingereza,Uholanzi,Ubelgiji,Hispania na Italia.
Wanunuzi wakubwa wa inta ya Tanzania ni Japani,Uholanzi,Marekani,Ujerumani na Ufaransa.

Soko la ndani la asali ni 10,000 mpaka 20,000/= kwa lita moja,Ambapo soko la nje ni wastani wa dola 4.5 kwa lita.
Tanzania kuna takribani wilaya 30 zinazohusika na ufugaji wa nyuki.
Baadhi ya wilaya hizo ni Manyoni,urambo,Lindi,Songea,Sikonge, na Chunya

Serikali ya Tanzania tayari imeandaa sera na mikakati kuhakikisha kua ufugaji wa nyuki unakua endelevu.Hii ni pamoja na kuanzisha upya chuo kinachotoa Astashahada na Stashahada za elimu ya nyuki kilichopo Tabora.

Serikali pia kwa miaka 2011/2012 na 2012/2013 imekua ikifadhili mizinga 5000 kila mwaka ktk baadhi ya wilaya hizi 30.

Mizengo Pinda Waziri Mkuu wa Tanzania ni Mdau mkubwa wa Ufugaji wa nyuki huko Katavi..
Somo la nyuki pia hufundishwa katika chuo kikuu cha  Sokoine Kilichopo Morogoro.

Endapo utahitaji msaada wowote jinsi ya Kuanzisha Ufugaji wa nyuki Tuwasiliane kupitia
+255768937884/balelefabian@yahoo.com




KULIA:Wanafunzi wa shahada ya kwanza ya Misitu Chuo kikuu cha Sokoine Morogoro wakishiriki mjadala ktk kituo cha televisheni cha Sua Tv Katika mada ya Ufugaji wa Nyuki unavyoweza kumkomboa Kijana iliyoandaliwa na TFSA(Tanzania Forestry Students' Association)











Fabian Frank Balele akibainisha changamoto za ufugaji wa nyuki katika mada hiyo.Ambapo miongoni mwa changamoto kubwa ni utayari wa vijana kujihusisha katika ufugajai wa nyuki,shughuli ambayo imekua haitiliwi maanai na vijana walio wengi kwa kupenda kazi za maofisini pekee.












                 Kundi kubwa la nyuki likiwa limejikusanya kwenye majani ya nyuki,Nyuki hawa wakiandaliwa mazingira ya ufugaji wanaweza kua chanzo kizuri cha ufugaji wa nyuki.Inakadiriwa kua kundi moja la nyuki lina uwezo wa kua na nyuki hadi 80,000 Ambapo Malkia hua ni mmoja tu ktk kundi hilo.



Mizinga ya Kienyeji ya Nyuki,Mizinga hii ndimo hutumiwa kama nyumba  ya nyuki katika ufugaji.
Asali nyingi ya Afrika inatokana na Mizinga ya Kienyeji kutoka na ile ya kisasa kua na bei ghali hadi kufikia 70,000/= kwa mzinga mmoja.








Mizengo Pinda Waziri Mkuu wa Tanzania akiweka jiwe la msingi katika mradi mpya wa ufugaji wa nyuki Mkoani Geita Kijiji cha Bugulula.
Kwa mbele ni Mizinga ya nyuki ya kisasa kwa ufugaji wa nyuki wa kisasa.



Mizengo Pinda akifungua jiwe la Msingi ktk Mradi wa Nyuki ulioko Kwimba Mkoani Mwanza.
Kwa nyuma kushoto ni mkewe Mama Tunu Pinda,Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarest Ndikilo.
Mizengo Pinda ni Mdau Mkubwa wa Ufugaji WA Nyuki Tanzania Nyumbani kwake Katavi.

Mazao ya Nyuki, Asali.
Chini kushoto ni Lotion Itokanayo na Inta ya nyuki.









                                                                 ASALI

WAJUE MATAJIRI WANOONGOZA AFRIKA,TANZANIA.

Habari za kuaminika kutoka ktk majarida ya The Forbes, Pan African Business,Ventures Afrika yanamtaja Said Salim Bakhresa kua ndiye tajiri wa kwanza Tanzania na anashika nafasi ya 30 kati ya matajiri 40 wa Afrika.
Gulam Dewji anafuatia akishika nafasi ya pili huku Rostam Aziz akishika nafasi ya 3,Reginald Mengi anashika nafasi ya 4 na wa tano ni Ali Mufuruki.

1.SAID SALIM BACKHRESA .

Anamiliki mali na fedha zenye thamani ya Dola za Marekani 620 Million sawa na Tsh.992 Bilion(Dola 1=1600)
Utajili wake unatokana na mapato yanayotokana na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kwenye viweanda vyake.
Inasemekana kua Bakhresa aliacha shule akiwa na miaka 14 miaka ya 1970 na kuanzisha shughuli zake za biashara ndogondogo za uuzaji wa Urojo Huko Zanzibar.
Baada ya mda alifungua Mgahawa,akanzisha mashine ya kusaga nafaka kisha akaanzisha viwanda vya usindikizaji wa vyakula kama vile mikate,kutengeneza chokolate,Icecream na vinywaji Baridi.

2 ALHAJ MOHAMED.GULAM DEWJI.

Ana mali na fedha zenye thamani ya Dola 560 Milion.
Ni sawa na Bilion 896 za Kitanzania.
Utajiri wa Dewji unatokana na kuzalisha bidhaa na kutoa huduma mbalimbali.
Anamiliki makampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania inayofanya kazi Afrika Mashariki na Kati,21st century Textile,Kampuni ya Bima,Makampuni ya kuuza mafuta ya Petrol na maduka mbalimbali zaidi ya 100 Tanzania.




3.ROSTAM AZIZ

Ana mali na fedha zenye thamani ya Dola 420Milion sawa na Tsh.672 Bilion.
Utajiri wake unatokana na kumiliki Hisa za makampuni ya mawasiliano ya simu,madini,Biashara za Usafiri wa Meli.
Anamiliki asilimia 19 ya Hisa za Kampuni ya Vodacom.
Amewahi kua mbunge wa Igunga kwa kupitia CCM Kuanzia mwaka 1995-2011.


4.REGINALD MENGI.
Ana mali na Pesa zenye thamani ya Dola 280 Milion. 
Sawa na Sh.448 Bilion.


Anamiliki Kampuni mbalimbali Ikiwemo vyombo mbalimbali(Ni Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP- Medi,yenye vyombo vya Habari vya ITV,RADIO ONE,EATV,EATV RADIO,CAPITAL RADIO,CAPITAL TELEVISION).
Anamiliki viwanda vinavyozalisha vinywaji Baridi vya Coca cola na Mgodi wa Dhahabu.

5. ALI  MUFURUKI.
Anamiliki mali na Pesa zenye thamani ya Dola 110 Milion(176 Bilion)
Utajiri unatokana na kazi ya Uendelezaji Makazi na Ukodishaji,Matangazo na Shughuli za mawasiliano.
Ni mkurugenzi wa Info Tech Investment LTD-Dar Es Salaam.
Ni mwenyekiti wa Mwanachi Communications LTD(yenye magazeti ya Mwananchi na The Citizen)
 NB:Wamepatikana kutokana na nafasi zao kifedha,ufanisi wa kampuni zao ktk soko la hisa,mfumo wa wanahisa ktk soko la hisa,na mtiririko mzima wab kifedha ktk kaunti zao kwenye benki mbalimbali.
Chanzo:Jarida la Ventures Afrika,jarida la Forbes,na jarida la Pan African Business.

KUPATA LIST YA MATAJIRI 40 WA AFRIKA 

Click:http://www.forbes.com/africa-billionaires/list/

Saturday, December 22, 2012

OPTICAL MARK READER(OMR)-TEKNOLOJIA ILIYOSAIDIA KUPUNGUZA UDANGANYIFU MTIHANI DARASA LA SABA-2012.

Teknolojia mpya ya usahihishaji wa mitihani kwa kutumia kifaa cha kisasa(Optical Mark Reader) imechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza udanganyifu katika mitihanai ya darasa la saba iliyofanywa Septemba mwaka huu
.
Akiongea kutoka katika ofisi za Wizara ya Elimu jijini Dar Es Salaam,Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa amebainisha kua Teknolojia hii imepunguza udanganyifu katika mitihani hiyo kwa kua ni watahiniwa 293 pekee kati ya 865,534 waliofanya mitihani mwezi Septemba mwaka huu wamefutiwa matokeo yao ikilinganishwa na watahiniwa 9,736 waliofutiwa matokeo yao kutokana na sababu za udanganyifu kwa mwaka jana.
OPTICAL MARK READER
  MATOKEO YA DARASA LA SABA 2012.ASILIMIA YA UFAULU YAONGEZEKA.
Sanjali na hilo Pia Dk.Kawambwa alibainisha kua kiwango cha ufaulu wa darasa la saba umepanda Kwa asilimia 8.8(8.8 %) .

Hata hivyo matokeo hayo si mazuri sana kwani zaidi ya nusu ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza  mwaka 2013 wamepata Ufaulu wa daraja D.
Jumla ya wanafunzi 294,833 sawa na asilimia 52 % ya wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wamepata daraja D.
Ambapo wanafunzi 265,873 sawa na asilimia 47.41% walifaulu kwa viwango vya madaraja ya A,B,C.

Mchanganuo wa matokeo ya jumla kwa kufuata madaraja ni kama inavoonesha hapa chini
 Daraja.      Idadi ya Wanafunzi.
A                   3087
B                  40683
C               222,103
D               526,397.
E                  73,264
Jumla wa wahitimu 560,706 kati ya 865,534 wamechaguliwa kujiunga na Sekondari Jan.2013.
Kati yao wasichana ni 281,460-sawa na asilimia 50.20%
Wavulana ni 279,246 -sawa na 49.80%.











Dk.Shukuru Kawambwa,Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi

Friday, December 21, 2012

LEMA MBUNGE HALALI WA ARUSHA MJINI.

Mahakama ya rufaa Tanzania imemthibitisha Godbless Lema kua ni Mbunge halalai wa Arusha Mjini baada ya kushinda rufani kufuatia kesi iliyofunguliwa dhidi yake ya kupinga ushindi wa ubunge wake kwa tuhuma kua alitumia lugha ya matusi na ubaguzi wa kijinsia katika moja ya mikutano yake wakati wa kampeni dhidi ya mpinzani wake Dk.Batilda Burian wa CCM.
.
 Akiongea kutoka ktk ofisi za Mahakama ya Rufaa Mh.Tundu Lisu ambae ni Mkurugenzi wa Haki na Sheria wa CHADEMA alidai kua malalamiko hayo ni batili kwa kua mawakili wa mlalamikaji wameshindwa kuthibitisha kua:

 1)Ni kwa jinsi gani mshtakiwa alitumia lugha ya matusi Na udhalilishaji wa kijinsia. 
2)Ni kwa jinsi gani lugha ya matusi iliwaathiri wapiga kura kupelekea kushawishika kutompigia kura Dr. Buriani,
Vilevile Alidai kua walalamikaji hawakuthibitisha kama walikua ni wapiga kura au wenye sifa za kupiga kura hivyo hawakua na sifa kisheria kufungua kesi hiyo.

 Godbless Lema alivuliwa ubunge wa Arusha mjini na Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha April 5 mwaka huu chini ya Jaji Gabriel Rwakibarila kufuatia tuhuma za walalamikaji,Musa Mkenga,Agnes Mollel na Hapiness Kivuyo,Waliofungua mashtaka mahakamani kupinga ushindi wa Godbless Lema kwa kua Alitumia lugha ya matusi na Uzalilishaji wa kijinsia. 

 Baada ya ushindi wa rufani hiyo Mahakama ya Rufaa imemtangaza Godblee Lema kua ni Mbunge Halali wa Arusha Mjini kupitia CHADEMA.  

 Makada wa CCM(Hapiness Kivuyo,Agnes Molel na Mussa Mkenga ) Waliofungua mashtaka ya kupinga ushindi wa Lema
Godbless Lema na wafuasi,viongozi wa CHADEMA wakishangilia ushindi wa rufani hiyo.

Sunday, December 16, 2012

WATU KADHAA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI SINGIDA KWA TUHUMA ZA KUTEKA GARI YENYE JENEZA LA MAREHEMU RYOBA MUNCHARI

Jeshi la Polisi mkoani Singida linawashikilia watu wapatao 25 kwa tuhuma za kuteka gari ndogo yenye maiti mali ya Chuo kikuu cha Sokoine(SUA) kilichopo mkoaniMorogoro.
.
Gari hiyo aina ya Land Cruiser iliyokua ikendeshwa na Bwn.Kastus Mapulila ilitekwa taehe 8/12/2012 kama ilivyoripotiwa na Balele Mwanahabari.

Akithibitisha kwa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi mkoani Singida Linus Sinzumwa amedai kua watuhumiwa hao wengi wao wanatoka kijiji cha Kisaki nje kidogo ya Manispaa ya Singida.

Aliendelea kuthibitisha kua baadhi ya mali zilizopatikana kwa watuhumiwa hao nio pamoja na laptop,kamera,simu za mkononi na nguo za wasindikizaji ktk msafara wa kusafirisha mwili wa Marehemu kuelekea Musoma mkoani Mara.
.
Inadaiwa kua watuhumiwa hao wamekamatwa kufuatia ushirikiano baina ya jeshi la polisi na wananchi baada ya watuhumiwa kulewa pombe na kudai kua wamepata pesa na hali zao kiuchumi zimeimarika.

Hatua za uchunguzi zinaendelea amabapo watuhumiwa watachujwa na baadhi kufikishwa mbele ya Sheria kujibu mashtaka yanayowakabili.

Jumla ya milioni 19 zilipokonywa katika tukio hilo la uvamizi wa msafara wa kusindikiza mwili wa Marehemu.

Marehemu Ryoba Munchari alikua mwanafunzi wa mwaka wa tatu kutoka chuo kikuu cha Sokoine(SUA)-Morogoro
Chanzo:Gazeti la Nipashe.

Gari iliyotekwa na majambazi huko Singida ikiwa imebeba mwili wa marehemu Ryoba Munchari mda mchache kabla ya safari kuanza kutoka Sua.

                                              Marehemu Ryoba Munchari enzi za uhai wake.
.

Saturday, December 15, 2012

MIKE TYSON AKANA UVUMI WA YEYE KUBADILI JINSIA

Takribani wiki 2 zilizopita sasa kumekuwepo na uvumi wa yule aliyekua Bondia wa uzito wa juu Duniani Mike Tyson kua amebadili jinsia na ataitwa Michelle.

Inadaiwa kua uvumi huo si wa kweli na habari za kukanusha uvumi huo zimethibitishwa na Mike Tyson mwenyewe na kuripotiwa na Shirika la utangazaji la BBC.

Inasemekana kua uvumi wa Mike Tyson kubadili  jinsia ulianzia kwenye website ya Satritical ya NewsBiscuit iliyoko inhini Uingereza mwishoni mwa mwezi November

Website ya NewsBiscuit handika makala mbalimbali za kubuni zisizo za ukweli na kuwahi kutokea.
Kwa kasi kubwa uvumi ulichochewa zaidi na makala mbalimbali za Afrika kwa kuanzia gazeti kubwa nchini Zimbabwe la The Standard  kisha kuendelea ktk website ya SpyGhana.

Kwa hapa Tanzania habari hiyo iliripotiwa na magazeti mbalimbali makubwa.
.
Kwa bahati mbaya zaidi Watanzania wengi wameendelea kudanganywa kua jambo hilo ni la ukweli huku magazeti mbalimbali yakiendelea kuripoti kua Sasa Mike Tyson ataitwa Michelle na tayari amepata Bwana.

                  Bondia wa zamani wa uzito wa Juu Duniani Mike Tyson aliyevumishiwa uvumi wa kubadili jisia.



Wednesday, December 12, 2012

PUMZIKA KWA AMANI"MUNCHARI RYOBA"

Tarehe 7/12/2012 sa 10:30 Alfajiri ulikua mda wa mwisho kuendelea kuvuta pumzi  kwa kipenzi chetu Ryoba Munchari Wa kitivo cha Elimu(Georgraphy&Biology)Hapa SUA.

Akieleza kwa masikitiko makubwa Rais wa Serikali ya wanafunzi Chuo kikuu cha Sokoine- SUA Bwn, IDD IDD,alieleza kua kifo cha Marehemu Ryoba Munchari kilitokea ghafla," Marehemu aliugua ghafla usiku huo na kukimbizwa hospitali ya chuo na mda mfupi baada ya kufikishwa hospitali akawa amekata roho."

Inasemekana kua mda mfupi kabla ya kifo chake Marehemu alikua ktk msongo wa mawazo baada ya mjane wa marehemu kujifungua kwa operation,paka kifo kinamkuta mjane wa marehemu alikua amelazwa hospitalini kutokana na kujifungua kwa operation.

Mwili wa Marehemu uliagwa rasmi tarehe 7/12/2012 mchana ktk ukumbi wa Freedom Square-SUA,na mda mfupi baada ya IBADA maalumu ya kumuombea Marehemu,mwili ulisafirishwa kuelekea mkoani Mara kwa ajili ya mazishi.

Marehemu alikua mwajiriwa wa shule ya sekondari LAMADI Mkoa wa SIMIYU na mwaka 2010 ndipo marehemu alipoanza masomo ya Shahada ya kwanza ya Ualimu.

Marehemu ameacha mjane na mtoto mmoja.

"BWANA ALITOA, BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE"


MAJAMBAZI WAVAMIA GARI LA WASINDIKIZAJI WA MWILI WA MAREHEMU

Katika hali isiyo ya kawaida Watu wanaosadikika kua majambazi wakiwa na bunduki aina ya Gobore na siraha nyingine za jadi walivamia gari lililokua likisindikiza mwili wa marehemu usiku wa tarehe 8/12/2012 Majira ya sa 7:30 kilomita chache kabla ya kuingia mjini Singida.

Akiongea kwa masikitiko makubwa Raisi wa serikali ya wanafunzi-SUA  Bwn  IDD IDD ambaye pia alikua katika msafara aldai baada ya kufika eneo la tukio walikuta mawe makubwa yamepangwa njiani na ndipo walipoamriwa kushuka nje na kuacha kila kitu walicho kua nacho,majambazi hayo yalifanikiwa kuchukua fedha zote walizokua nazo,mabegi ya nguo,simu,computer ndogo(laptop)pamoja na vitu vingine walivyokua navyo
.
Vili vilie wasindikaizaji hao walijeruhiwa sehemu mbalimbali kupelekea kufikishwa katika hospitali ya mkoa-SINGIDA kwa ajili ya matibabu
.
Kama hiyo haitoshi, majambazi hayo yalibomoa jeneza alimokua amehifadhiwa maiti kwa kudhani kua kutakua na pesa iliyo kua imeficha humo.

Baada ya tukio hilo mawasiliano yalifanyika na gari nyingine ilitumwa kutoka SUA kwa ajili ya kuendelwa na safari ya kuasafirisha mwili wa marehemu Ryoba Munchari.
GARI YA MSALABA MWEKUNDU IKIWASILI KTK UKUMBI WA FREEDOM SQUARE-SUA NA MWILI WA MAREHEMU RYOBA MUNCHARI TAYARI KWA KUANZA IBADA YA KUMUOMBEA MAREHEMU.




WANAFUNZI WA SUA WAKIWA WAMEJIANDAA KULIPOKEA JENEZA LA MAREHEMU
                                    





   MUOMBOLEZAJI AKIWA NA PICHA  YA MAREHEMU RYOBA MUNCHARI






JENEZA LENYE MWILI WA MAREHEMU RYOBA MUNCHARI LIKIWA MBELE YA UKUMBI WA FREEDOM SQUARE TAYARI KWA IBADA MAALUMU YA KUUAGA MWILI

































Monday, December 3, 2012

VIJANA WASOMI WAASWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KTK MABADIRIKO YA KULINDA RASILIMALI ZA NCHI

Vijana wa vyuo vikuu wameaswa kua mfano ktk jamii ili kutetea na kulinda Rasilimali za nchi hii,kauli hizo zimetolewa na viongozi na Wabunge mbalimbali ktk Kongamano lililohusisha vijana wa CHADEMA vyuoni- Mkoani Morogoro,

Akiongea kwa masikitiko makubwa Mbunge wa Morogoro viti maalumu kwa tiketi ya CHADEMA Bi. Suzan Kiwanga,alidai kua viongozi wengi wa sasa wanajali maisha yao kwa kujilimbikizia mali na kuwasahau wananchi walio sehemu kubwa ya Taifa letu.

Nae Mbunge wa viti maaalumu wa Hanang, Manyara  Bi Rose Kamili aliwaomba vijana wa kike kushiriki ipasavyo katika masuala ya siasa kwani asilimia kubwa ya wasichana na wanawake kwa ujumla hawapendi siasa.

Alidai kua harakati za siasa haziepukiki kwani ktk nchi yetu bado tunamfumo wa kupata viongozi kupitia siasa na tusipokua makini wakati wa kuchagua viongozi watu wasiofaa watashika madaraka na kusababisha matatizo mbalimbali kwa kutokuwajibika.

Alizidi kusema kua vijana wajitokeze ktk kugombea nafasi mbalimbali za uongozi hasa udiwani kwani idadi kubwa ya madiwani ktk nchi hii hawana sifa za kuwawezesha kufanya maamuzi mazuri kutokana na elimu ndogo waliyo nayo.

Nae katibu wa BAVICHA(Baraza la Vijana Chadema)Taifa, Deo Munishi alielezea kwa undani kuhusiana na Falsa,Itikadi na Sera za CHADEMA na kuwaasa vijana kisoma kwa umakini katiba ya CHADEMA ili kuwaelimisha wananchi wa kawaida ambao wengi wao hawaijui katiba hiyo.

Aliendelea kwa kusema kua anasikitishwa na kitendo cha baadhi ya wanasiasa hapa nchini kwa kupotosha sera ya MAJIMBO ya CHADEMA kua ina lengo la kuwagawa Watanzania,Alidai kua kufikiri hivyo ni hali ya kua na upeo mdogo wa kufikiri kawani sera hiyo ina lengo la kuleta umoja na kuharakisha maendeleo kwa wanchi tofauti na baadhi ya wanasiasa ambao wamekua wakipotosha sera hiyo.
.
Nae Mchungaji Peter Msigwa a.k.a Mzee wa Falsafa mbunge wa Iringa Mjini  alidai kua vijana wajikomboe kifikra kwanza ndipo waweze kutaka kusimamia rasilimali za Taifa hili,aliongea kwa msisitizo huku akinikuu kauli mbalimbali za wasomi na wanafalsafa wa kale kama kama vile: "Problems can not be solved by the same level of thinking that created them"" Change what you think by changing what you see"

Alidai kua vijana kupitia CHADEMA hawatakua na maana yoyote iwapo watapata nafasi za uongozi na kuendelea kufanya madudu yale yale,vijana hasa Wasomoi wa chuo kikuu wanatakiwa kua chanzo cha kutafuta suruhisho la matatizo yanayowasibu wananchi wa kawaida na si kubaki kulalalamika  siku zote
.
Nae Mwenyekiti wa Bavicha Taifa-Ndg.JOHN HECHE alimalizia kwa kusema kua vijana wanatakiwa kujitoa kikamilifu ktk mapambano ya kupinga vitendo vya rushwa,tamaa ya madaraka,ubadhirifu,ufisadi na maovu mengine yaliyo kinyume na maadili ya Uongozi kwa nguvu zote kila siku bila kuogopa.

Kongamano hilo liliandaliwa na umoja wa vijana wa vyuo vikuu-CHADEMA(CHASO) kupitia Mkoa wa Morogoro.
                         Vijana kutoka SUA wakiwasili ktk hotel ya SARVOY  kwa ajili ya kushiriki ktk kongamano hilo.


viongozi wa CHASO(Morogoro)
Wakifatilia kwa makini mada zilizokua zikiwasilishwa ktk kongamano hilo.





Kulia-vijana kutoka vyuo mbalimbali wakifatilia kwa makini mada mbalimbali .
Kulia-Mbunge wa Hanang' Rose Kamili akiwasilisha mada ya mchango wa Vijana wa kike katika Siasa.
                   Mchungaji Peter Msigwa Mbunge wa Iringa mjini                akisisitiza jambo katika Kongamano hilo.
                                      John Heche-M/kiti BAVICHA akihitimisha kutoa mada katika kongamano hilo.
Kulia juu Mbunge wa Morogoro-CHADEMA,Bi Suzan Kiwanga,na Salvatory Machemli(kulia chini) mbunge wa Ukerewe wakimpongeza Balele Mwanahabari kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuihabarisha jamii ktk masuala mabalimbali.