Friday, November 30, 2012

RAIS UDOM KUCHUNGUZA TUHUMA ZA UKAHABA CHUONI HAPO

Rais wa serikali ya wanafunzi ya Chuo kikuu cha Dodoma(UDOM)-UDOSO, Bwn. Paul Yunge,ameanzisha tume maalumu ya kuchunguza wanaojihusisha na ukahaba chuoni hapo,hali hiyo

Hali hiyo imefuatiwa baada ya vyombo vya habari kuripoti kua kuna baadhi ya wasichana chuoni hapo wanajihusisha na ukahaba ktk mitaa mbalimbli mjini DODOMA

Bwn Yunge amedai kua ni fedheha kubwa kwa wasomi wetu kujihusisha na vitendo vibaya vilivyo kinyume na maadili ya mtanzania
                          "Tunafanya uchunguzu kubaini ukweli wa tuhuma hizi,kwa watakaobainika              watachukuliwa hatua kali za kinidhamu kwa kua ni aibu kubwa kwa chuo kizima,wazazi na watanzania kwa ujumla"

SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE 28TH GRADUATION CEREMONY

TAR 23/12/2012 Kumefanyika  mahafali makubwa ya 28 chuo kukuu  Sokoine Morogoro ktk ukumbi wa Freedom Square,kampasi ya Solomon Mahlangu-Mazimbu.
Katika mahafali hayo yaliyoongozwa na Mkuu wa chuo (Hon.Al Noor Kassum),jumla ya wahitimu 1870 walitunukiwa Astashahada(certificates),Stashahada(diploma),shahada za kawaida(Bachelor degree),shahada za uzamili(Masters),na Shahada za udaktari wa Falsafa(PhD) mbalimbali zitolewazo chuoni hapo.

ALL GRADUANDS
MALE
FEMALE
TOTAL
1
UNDERGRADUATES
1114
451
1565
2
NON DEGREE PROGRAMS(Dipl.in Records Archives&infor Mgt,Dipl in Information&Library Sciences
57
54
111
3
Masters Programs
128
43
171
4
PhD Programs
12
11
23

TOTAL
1311
559
1870

                                        MATUKIO  KATIKA PICHA

MABADIRIKO YA KONGAMANO LA VIJANA -MOROGORO

Lile kongamano kubwa la vijana Morogoro,lililokua lifanyike tar 1/12/2012 sasa kufanyika 2/12/2012 kuanzia sa 3-8 mchana. Savoy main Hall, na si Forest Hill Sec.School hall kama ilivyoelezwa hapo mwanzo. mabadiriko hayo yamefanywa na uongozi wa umoja wa chadema vyuo vikuu(CHASO)MOROGORO kutokana na sababu mbalimbali,
Mada kuu ktk kongamano hilo ni pamoja na:
1)Ushirika wa vijana ktk siasa kwa maendeleo ya Taifa
2)Mtazamo wa vijana juu ya usimamizi wa Rasilimali za Taifa
3)Kuporomoka kwa uchumi wa Taifa na athari zake  kwa vijana
4)Matumizi mabaya ya nguvu za nguvu za dola ktk siasa na athari zake kwa maendeleo ya Taifa.
Vijana mbalimbali kutoka vyuo vikuu Morogoro wanatarajiwa kuhudhuria ktk kongamano hilo.
Vijana kutoka-Sokoine university,Mzumbe university,Jordan University,Muslim university,Ardh,Liti-Morogoro,MSJ-Morogoro na Ujenzi college, wanatarajiwa kuhudhuria.
Wasemaji wakuu wakiongozwa na Aliyekua Mbunge mwanaharakati wa Arusha mjini Bwn Godbless lema ni pamoja na
1)Godbless Lema-Aliyekua mbunge-Arusha mjini
2)Mchungaji Peter Msigwa-Mzee wa falsafa, Mbunge-Iringa Mjini
3)John Heche-M/kiti-Bavicha
4)Munish Deo-katibu Bavicha
5)Rose Kamili-Mbunge
6)Susan Kiwanga-Mbunge
GODBLESS KEMA
Mch.Peter Msigwa
John Heche


Monday, November 26, 2012

R.I.P SHARO MILLIONAIRE

SHAROBARO KULIA AKIWA NA MZEE MAJUTO ENZI ZA UHAI WAKE KTK MOJA YA TUZO
Habari za kuaminika kutoka Muheza Mkoani Tanga zinasema kua yule Muigizaji na Mwanamuziki maarufu hapa nchini Hussein Ramadhan Mkieti a.k.a Sharo Millionaire amefariki Dunia jana usiku 26  Nov 2012 saa 2 usiku katika ajali ya gari KTK Kijiji cha LUSANGA Muheza Tanga alipokua akielekea nyumbani kwao Mkoani Tanga.Habari hizi zimethibitishwa na kamanda wa polisi mkoani Tanga,Constatine Masawe.
MWILI WA SHARO BAADA YA KUPATA AJALI
SHARO MILLIONAIRE ENZI ZA UHAI WAKE

Saturday, November 17, 2012

TFSA WELCOME FIRST YEAR PARTY PALIKUA HAPATOSHI

Hayawi hayawi mwishowe yakawa,ile siku ambayo watu wengi wallisubiri ili kushehereka pamoja kama familia moja ya wataalamu watarajiwa wa misitu,ilifikia kikomo rasmi siku ya jana tar 16/11/2012 katika hotel maarufu mjini Morogoro-SAVOY HOTEL.
Kama ni asilimia basi nadiriki kusema kua ilikua ni aslimia 99 na kama ni furaha basi ni zaidi ya yote.
Tafrija hiyo ilifanyika chini ya Uongozi wa Tanzania Forestry Students'Association(TFSA)
Shughuli ilianza rasmi mida ya sa moja jioni ambapo washiriki walionekana wapya kutokana na vikali walivyokua wametupia huku baadhi wakiibuka kua super stars wa siku,
washiriki wote walikula na kunywa ipasavyo huku brudani ikitawala.shughuli ilikamilika rasmi majira ya sa 6:30 usiku huku baadhi ya washiriki wakitamani brudan iendelee paka asubuhi
Katika hotuba yake Mgeni rasmi Dr. Dos Santos aliwahakikishia wataalamu watarajiwa wa misitu kua wapo ktk upande sahihi hivyo wasiwe na wasiwasi katika suala la ajira kwa kua suala la misitu ni endelevu lenye tija katika nchi yetu na duniani kwa ujumla kutokana na mikakati ya uhifadhi wa mazingira
Pia mgeni rasmi aliishauri TFSA kuhakikisha kua inabuni miradi mbalimbali ili kujiimarisha kiuchumi
Sanjari na hayo pia kulifanyika mchango maalumu wa kujenga mfuko wa TFSA ambapo jumla ya Tsh.453,000/=. zilipatikana.
washiriki wakiwasili SAVOY HOTEL tayari kwa kuanza shughuli ya kushehereka
Hapa ukumbi ulipendeza sana baada ya kupambwa na wanadada wenye mafunzo ya upambaji kutoka China.
Mwanadada Milkajeni Sangiwa akiwasili ukumbini na keki maridadi kabisa yenye viwango vya kimataifa


Hii pair ilimvutia kila mtu mahali pale,Bwn Oscar akiwa na Pertner wake ktk zero distance
Vinywaji kila aina vilipatikana
Mda si mrefu waggling ikaanza kama ishara ya ufunguzi wa tafrija hiyo
Vijana washehereshaji wakifanya mambo yao jukwaani
Waggling ikiendelea
HAPA VIJANA WALIOPENDEZA ZAID WAKIWA WAMEICHAFUA MEZA
VIJANA WATANASHATI WAKIWA WAMEPENDEZA VILIVYO
MGENI RASMI DR.SANTOS(WA PILI KUSHOTO)MKUFUNZI KUTOKA SUA MR.KILAWE(WA KWANZA KUSHOTO),MWENYEKITI WA TFSA(BWN. SHADRACK MFILINGE)NA DADA JANE WAKIWA WAMEICHAFUA MEZA VILIVYO)
VIJANA WATANASHATI CHINI YA KAJIN MASTER a.k.a MR.KIDUKU KTK POZI
KATIKA SHAMRA SHAMRA HAPAKOSI VITUKO VYA HAPA NA PALE
WASHIRIKI WALIKULA NA KUNYWA MPAKA BASI.
BAADA YA CHAKULA BRUDANI KAMA KAWAIDA,ILIKUA NI WAGGLING DANCING KWA KWENDA MBELE

BRUDANI IKIENDELEA,



MHADHARA WA KUMBUKUMBU YA HAYATI SOKOINE WAFANYIKA CHUO KIKUU CHA KILIMO SOKOINE MOROGORO

Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal alikua Mgeni rasmi na Msemaji mkuu  ktk Mhadhara wa 13 wa kumuenzi Hayati Moringe Sokoine uliofanyika jana tar 16 Nov.2012 Katika ukumbi wa Freedom Square ulioko chuo kikuu cha Kilimo Sokoine(SUA)  Morogoro ktk CAMPUS ya Solomon Mahlangu.
Katika mhadhara huo,wageni mbalimbali na wanataaluma wakiwemo pia wanafunzi wa chuo hicho walipata nafasi ya kujumuika pamoja na kusikiliza hotuba iliyotolewa na Msemaji mkuu Dr. Gharib Bilal.
Miongoni mwa wageni hao alikua ni Mkuu wa chuo hicho(Al Noor Kassum) na makamu wake(Prof.Monela),wakuu mbalimbali wa idara za chuo,Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Naibu waziri wa Elimu,Mkurugenzi wa Elimu ya Juu na wengine wengi.
Katika hoyuba yake Dr. Bilal aliwaasa wasomi wa Tanzania kujichunguza kama kweli wanamuenzi Hayati Sokoine kwa vitendo na si nadharia.
Mmoja wa wanachuo aliyepata nafasi ya kumuuliza Msemaji mkuu wa mhadhara Dr. Bilal
Wanafunzi wa chuo hicho pia walipata nafasi ya kumuuliza msemaji mkuu Dr. Bilal maswali
mbalimbali.
Wanachuo kutoka SUA wakisikiliza hotuba ya Msemaji mkuu wa Muhadhara Dr.Galib Bilal
Makamu wa Rais Tanzania Bara Dr. Bilal akijibu maswali yaliyoulizwa na mmoja wa wageni ktk mhadhara huo
Prof fessor Ngaga,Dean of faculty of Forestry and Nature Conservation(katikati)Balele Mwanahabari(kushoto)na Mr.Gaston Buberwa mara baada ya mhadhara
Makamu wa Rais akipokea zawadi maalumu kutoka kwa Mkuu wa chuo hicho(Al Noor Kassum) ya bidhaa zinazotengenezwa ktk Chuo kikuu cha Sokoine,(baadhi ya bidhaa hizo ni kalamu,vitabu,T-shirts na kofia)
WANACHUO KUTOKA SUA

MBOWE MGENI RASMI KATIKA KONGAMANO LA WANAVYUO-MOROGORO

Mwenyekiti wa Chama Cha  Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA)/Mbunge wa HAI,ambaye pia ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni Bwn, Freeman Mbowe,anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi ktk Kongamano kubwa la wanavyuo vikuu hapa Mjini Morogoro,balelemwanahabari.blogspot.com imeelezwa.
Kongamano hilo litakalohusisha wanavyuo kutoka Sokoine,Mzumbe,Muslim University,na vyuo vingine linatarajiwa kufanyika tar 1 desemba 2012 ktk ukumbi Uliopo Forest Hill Sec School.
Habari za kuaminika zinasema kua Bwn Freeman Mbowe ataambatana na Wbunge wengine vijana wa chama hicho kutoka majimbo mbalimbali hapa Tanzania.
List kamili ya Wabunge hao inatarajiwa kutajwa mda wowote kuanzia sasa,ambapo balelemwanahabari.blogspot.com itakujuza mara moja kuhusiana na list ya wabunge hao.
                                 Freeman Mbowe Mwenyekiti wa CHADEMA
Mh. Mbowe Katika moja ya Harakati zake
Miongoni mwa hoja za msingi ni Pamoja na kuamsha hali ya siasa kwa wanavyuo ambao pia ni wasomi na viongozi watarajiwa, sanjali na hilo zoezi la kuwakaribisha mwaka wa kwanza kwa vyuo vyote litakua ni miongoni mwa shughuli ya msingi.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) ndicho chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania

Tuesday, November 13, 2012

MAANDALIZI YA SHEREHE TFSA WELCOME FIRST YEAR YAPAMBA MOTO

Maandalizi ya sherehe kwa ajili ya welcome first year TANZANIA FORESTRY STUDENTS ASSOCIATION(TFSA) yamepamba moto,Balelemwanahabari.blogspot.com imethibitisha.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati za maandalizi ya sherehe hiyo Bwn,OYUGI kutoka SUA Forestry class year 3,amethibitisha kua mpaka sasa wanategemea kua na wageni wasiopungua 100.
Ameeleza kua sherehe hiyo inatarajiwa kua ya kiutofauti ukilinganisha na sherehe nyingine za nyuma na zaidi ya sherehe za association nyingine HAPA SUA.
Mwenyekiti wa TFSA Bwn Shadrack Mfilinge amedai kua "unajua ndg yangu Balele Mwanahabari,TFSA ni Association kubwa na yenye nguvu hapa SUA kutokana na Uongozi thabiti Ukilinganisha na association nyingine"Hivyo basi inatakiwa pia kuonesha kua sisi ni watu makini na very strong ktk utendaji kwa kila jambo likiwemo suala la sherehe hii.

Nae Makamu mwenyekiti wa TFSA Bwn Lazaro Nko amedai kua wanataraja kua na wageni mbalimbali wakiwemo wakufunzi wakuu Senior professors and Doctors wasiopungua10,kutoka ktk kitivo Cha misitu.

Mchango wa sherehe hiyo umetajwa kua ni Tshs.12,000/= Na sherehe hiyo inatarajiwa kufanyika tarehe 16/11/2012 siku ya J MOSI Katika Hotel maarufu-SAVOY uliyoko Mjini Morogoro.
 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya sherehe hiyo Bwn Oyugi akiwa na Katibu wake ktk moja ya vikao vya maandalizi ya sherehe hiyo
 Wanakamati wakifatilia kwa makini moja ya kikao cha maandalizi ya sherehe hiyo ktk ukumbi wa Roundcafeteria SUA
                                                   Wanakamati ktk moja ya vikao
Mr.Ali Juma(kulia)- FACULTY representative akifatilia kwa makini ktk moja ya vikaohivyo.

Viongozi wa TFSA, Makamu mwenyekiti  na Katibu mkuu wakifatilia kwa makini ktk moja yakikao hicho
Viongozi Wa TFSA(Mwenyekiti,Makamu mwenyekiti na Katibu mkuu) wakifatilia kwa makini ktk moja yakikao
Mr.Obadia ktk moja yakikao

                                                                     Wanakamati



                              wanakamati wakifatilia kwa makini mchanganuo wa gharama za sherehe hiyo    

Sunday, November 11, 2012

MFUMO SAFI WA SISA MAREKANI UMESAIDIA KUMPATA RAISI KWA AMANI.
Kwa mara nyingine tena Barack Obama ameshinda kua Raisi wa Marekani kwa miaka minne mbele.
Obama ameshinda kua Raisi licha ya kukabiliwa na upinzani mkubwa wa chama cha Republican chini ya mgombea wake Bwn Mitt Romney.
Obama ameshinda kua Raisi baada ya kupata kura 270 za Electrol college zilizohitajika ili kupata ushindi,
kula hizo hupigwa na watu maalumu wanaoteuliwa na majimbo kulinga na idadi ya watu wa miji katika majimbo hayo.
Katika kura za jumla za wanachi zilizo muhimu kisiasa ambazo sizo zinazompa rais ushindi Obama alipata asilimia 50 dhidi ya 48 ya mshindani wake Mitt Romney.
MAREKANI ni nchi ya kuigwa Duniani kwa kuendesha kampeni nzuri na uchaguzi usiokua na dosari nyingi ikilinganishwa na AFRIKA.
Mara nyingi AFRIKA chaguzi nyingi huingiwa na dosari na kupelekea uvunjifu wa amani.
Hata hivyo Obama ameahidi kushirikiana na Romney katika sera zake ili kuijenga Marekani baada ya shughuki hizo za Uchaguzi.

                                    Rais Barack Obama ktk Hotuba yake ya ushindi.

                                                      Katika shrerehe za ushindi wa Obama
JK: MHASHAMU BALINA ALIKUA MDAU MKUBWA WA ELIMU;
 
 
Raisi kiwete akitia saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba ya aliyekua askofu wa jimbo kuu la Shinyanga Aloysius Balina aliyefariki tar 6/11 na kuzikwa jana tar 10/11/2012 katika kanisa la Mama wa Huruma Parokia ya Ngokolo MJINI Shinyanga.


Raisi Kikwete amesema kua Mhashamu Balina alikua mdau mkubwa wa elimu hapa nchini.
Raisi amesema hayo jana ktk mazishi ya aliyekua Askofu mkuu wa jimbo la Shinyanga Aloysius Balina mjini yaliyofanyika  katika kanisa la Mama wa Huruma Parokia ya Ngokolo Mjini Shinyanga,Aliyefariki tar 6 nov 2012.
Raisi Kikwete akiweka mchanga katika kaburi la Mhashamu Aloysius Balina.

Mbali ya Raisi Kikwete,Mama Maria Nyerere na Raisi wa awamu ya tatu ndg,Mkapa pia walihudhuria mazishi hayo ya Mhashamu Aloysius Balina