Monday, November 5, 2012

JE,OBAMA ATATETEA KITI CHAKE HAPO KESHO?

Macho na masikio ya watu ulimwenguni kote ni kuhusiana na uchaguzi wa kiti cha Uraisi nchini Marekani Hapo kesho..
Kwa hali isiyo ya kawaida Mtetezi wa kiti hicho cha Uraisi  Barack Obama wa chama cha Democratic Anatarajiwa kuchuana vikali na Mgombea wa chama cha Republican Bwana Mitt Romney.
Mitt Romney amekua akimshutumu Rais Obama kwa kushindwa Kuifikisha Mrekani Katika hali nzuri ya Kiuchumi huku akidai kua ameshindwa kutatua masuala ya Ukosefu wa ajira kwa vijana.
wagombea uraisi nchini Marekani Rais Barack Obama Na Mpinzani wake Bwn. Mitt Romney


Hata hivyo Rais Barack Obama amekua akiwaambia Wamarekani kua Wampe tena nafasi ya kuiongoza Marekani Ili aendelee kutekeleze ahadi zake ambazo kwa kiasi kikubwa amezifanikisha.

No comments:

Post a Comment