Sunday, November 11, 2012

MFUMO SAFI WA SISA MAREKANI UMESAIDIA KUMPATA RAISI KWA AMANI.
Kwa mara nyingine tena Barack Obama ameshinda kua Raisi wa Marekani kwa miaka minne mbele.
Obama ameshinda kua Raisi licha ya kukabiliwa na upinzani mkubwa wa chama cha Republican chini ya mgombea wake Bwn Mitt Romney.
Obama ameshinda kua Raisi baada ya kupata kura 270 za Electrol college zilizohitajika ili kupata ushindi,
kula hizo hupigwa na watu maalumu wanaoteuliwa na majimbo kulinga na idadi ya watu wa miji katika majimbo hayo.
Katika kura za jumla za wanachi zilizo muhimu kisiasa ambazo sizo zinazompa rais ushindi Obama alipata asilimia 50 dhidi ya 48 ya mshindani wake Mitt Romney.
MAREKANI ni nchi ya kuigwa Duniani kwa kuendesha kampeni nzuri na uchaguzi usiokua na dosari nyingi ikilinganishwa na AFRIKA.
Mara nyingi AFRIKA chaguzi nyingi huingiwa na dosari na kupelekea uvunjifu wa amani.
Hata hivyo Obama ameahidi kushirikiana na Romney katika sera zake ili kuijenga Marekani baada ya shughuki hizo za Uchaguzi.

                                    Rais Barack Obama ktk Hotuba yake ya ushindi.

                                                      Katika shrerehe za ushindi wa Obama

No comments:

Post a Comment