Saturday, November 17, 2012

MBOWE MGENI RASMI KATIKA KONGAMANO LA WANAVYUO-MOROGORO

Mwenyekiti wa Chama Cha  Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA)/Mbunge wa HAI,ambaye pia ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni Bwn, Freeman Mbowe,anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi ktk Kongamano kubwa la wanavyuo vikuu hapa Mjini Morogoro,balelemwanahabari.blogspot.com imeelezwa.
Kongamano hilo litakalohusisha wanavyuo kutoka Sokoine,Mzumbe,Muslim University,na vyuo vingine linatarajiwa kufanyika tar 1 desemba 2012 ktk ukumbi Uliopo Forest Hill Sec School.
Habari za kuaminika zinasema kua Bwn Freeman Mbowe ataambatana na Wbunge wengine vijana wa chama hicho kutoka majimbo mbalimbali hapa Tanzania.
List kamili ya Wabunge hao inatarajiwa kutajwa mda wowote kuanzia sasa,ambapo balelemwanahabari.blogspot.com itakujuza mara moja kuhusiana na list ya wabunge hao.
                                 Freeman Mbowe Mwenyekiti wa CHADEMA
Mh. Mbowe Katika moja ya Harakati zake
Miongoni mwa hoja za msingi ni Pamoja na kuamsha hali ya siasa kwa wanavyuo ambao pia ni wasomi na viongozi watarajiwa, sanjali na hilo zoezi la kuwakaribisha mwaka wa kwanza kwa vyuo vyote litakua ni miongoni mwa shughuli ya msingi.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) ndicho chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania

No comments:

Post a Comment