Lile kongamano kubwa la vijana Morogoro,lililokua lifanyike tar 1/12/2012 sasa kufanyika 2/12/2012 kuanzia sa 3-8 mchana. Savoy main Hall, na si Forest Hill Sec.School hall kama ilivyoelezwa hapo mwanzo. mabadiriko hayo yamefanywa na uongozi wa umoja wa chadema vyuo vikuu(CHASO)MOROGORO kutokana na sababu mbalimbali,
Mada kuu ktk kongamano hilo ni pamoja na:
1)Ushirika wa vijana ktk siasa kwa maendeleo ya Taifa
2)Mtazamo wa vijana juu ya usimamizi wa Rasilimali za Taifa
3)Kuporomoka kwa uchumi wa Taifa na athari zake kwa vijana
4)Matumizi mabaya ya nguvu za nguvu za dola ktk siasa na athari zake kwa maendeleo ya Taifa.
Vijana mbalimbali kutoka vyuo vikuu Morogoro wanatarajiwa kuhudhuria ktk kongamano hilo.
Vijana kutoka-Sokoine university,Mzumbe university,Jordan University,Muslim university,Ardh,Liti-Morogoro,MSJ-Morogoro na Ujenzi college, wanatarajiwa kuhudhuria.
Wasemaji wakuu wakiongozwa na Aliyekua Mbunge mwanaharakati wa Arusha mjini Bwn Godbless lema ni pamoja na
1)Godbless Lema-Aliyekua mbunge-Arusha mjini
2)Mchungaji Peter Msigwa-Mzee wa falsafa, Mbunge-Iringa Mjini
3)John Heche-M/kiti-Bavicha
4)Munish Deo-katibu Bavicha
5)Rose Kamili-Mbunge
6)Susan Kiwanga-Mbunge
GODBLESS KEMA |
Mch.Peter Msigwa |
John Heche |
No comments:
Post a Comment